SIR JEFF⚡🇹🇿
SIR JEFF⚡🇹🇿

@Sirjeff_D

10 Tweets 2 reads Mar 05, 2024
🎙BUNGE LA VIJANA🎙
Quick summary japo niliwahi kulala
-Unaniruhusu kuchana mikeka ya watu leo? Unajua sisi ndio wale majobless, hatuna kazi ila tuna kitu?
-Kwenye maisha bila mentor huwezi kutoboa, kwasababu unachosoma chuo na unachokutana nacho mtaani ni vitu viwili tofauti
-Kwa mujibu wa sheria kuna aina 3 za mikataba ya kazi/ajiri na mwajiri lazima akupe mkataba, si hisani, si ombi, ni sheria
-Ukipata shida yoyote kazini, unatakiwa kuiReport ndani ya siku 30 kwa idara ya kazi na sheria - wana offices kila mkoa
-Likizo ni haki ya mfanyakazi yyt
-Kila m/kazi ana haki ya kuumwa au kuuguza🤣. Unatakiwa kupewa likizo ya siku 4 bila masharti
-Kama ni likizo lazima uiombe kwa maandishi, usipofanya hivyo - hiyo imeenda na maji.
-Kuna emergency leave na sick sheet na light duty unayopewa na daktari
-Watu hawajui hivi vitu
-Ukiwa mtoro kazini, makampuni ya kibongo bongo wao wanachowaza ni termination tu. Ni makosa sana!
-Aina ya mikataba kuna
i) wa muda maalumu (12 months)
ii) wa kazi maalumu (mfn fundi wa AC au vibarua wa kazi fulani
iii) Ns, usiokua na kikomo, yani hadi utakapokufa au kustafu
-Likizo ya uzazi kwa dada zetu ni siku 84 kwa mtoto mmoja, ama siku 100 kwa mapacha (mara 1 kwa kila miaka mitatu)
-Kwa wanaume bana, unaweza kuchukua likizo ya uzazi hata mara 50, uweze tu kuthibitisha kuwa mtoto ni wako.
-Kamwe usithubutu kusema "Mimi naacha kazi" ...
... ukifanya hivyo, unafukia haki na stahiki zako zote na utatakiwa kumlipa mwajiri wako mshahara wa mwezi mmoja
-Utaratibu wa kumwachisha mtu kazi ni lazima atumiwe notice siku 28, sababu lazima iainishwe kwanini anaachishwa kazi
-Kiinua mgongo ni hesabu ya muaka 10 ktk ajira
-Ukiachishwa kazi ni lazima upewe certificate of service na termination letter
-Mtu mwenye taaluma mfn accountant, lawyer, daktari... Hua mikataba yao ni ya miaka miwili - miwili
-Wafanyakazi wengi hawajui Workers Compensation Fund inavyofanya kazi. Ila huu mfuko una mchango sn
-Ukipata ulemavu/ugonjwa au ukawa unfit ukiwa kazini, lazima ulipwe mshahara kila mwezi hadi siku utakaporudi ktk mfumo
-Tukikupa mkataba wa kazi, tunakuchora tu kama unausoma, ukikurupuka tu kumwaga sign, umejifunga, yani hata tukikuhamishia Kakonko, utajigharamia kila kitu.
-Meza lazima zipinduke, zisipopinduka meza tutapinduka sisi
-Ishu za kazi zina changamoto nyingi, mara zote HR na mwajiri ni kitu kimoja, kiuhalisia mwajiriwa lazima aumie
-Kuna kitu kinaitwa "white elephant project🐘" mfn ofisi yote inaungua, hapo huwezi kuomba compensation.
-Kama ajira yako imesitishwa kabla ya miezi 12 tangu uajiriwe, huna uhalali wa kulipwa kiinua mgongo.
Sijui nini kiliendelea kwenye space baada ya hapa, sababu nilipitiwa na usingizi... nimekuja kuamka saa 10 usiku, simu yangu ikiwa imekata charge.
Leo tutaendelea tulipoushia.

Loading suggestions...