SIR JEFF⚡🇹🇿
SIR JEFF⚡🇹🇿

@Sirjeff_D

12 Tweets 15 reads Feb 05, 2024
ZETU DAGAA, KUKU TAMAA!
Tohora mzaliwa wa Bagamoyo, mtoto wa kishua mzee wake alikua m/kazi wa Ikulu na ubalozini
Kufika miaka 31 alioa Mkenya, wakaishi nchi mbalimbali km Ujerumani, Italy & Kenya
Tohora alipokua akija TZ alikutana na Sarah, binti mdogo m/funzi wa Zanaki
UZI🧵
1/ (Based on True Story)
Penzi la Tohora na Sarah likapamba moto, na kufanikiwa kupata watoto watatu; Happy, Simba na Blandina
Ktk kutafuta maisha Sarah akapata kazi Bank ya NBC, kutokana na juhudi na weledi akapanda vyeo hadi kuwa msimamizi wa fedha za kugeni
2/
Tohora akamchombeza Sarah kuhusu mchongo mmoja, kwamba atafute passports yake na watoto ila ziwe na majina bandia.
Uhuni ulichezwa, Sarah apata passport ndani ya siku15. Yake ikiwa na jina Khadija na za wanae zikiwa na majina Jamila, Halfan na Jennifer.
Kwanini walifany hiv
3/
Kumbe Tohora & Sarah walisuka mpango wa kupiga pesa bank
Ndani ya siku 5 Sarah alipiga almost £400,000 (TZS 1.3B) hizi ni pesa nyingi sn leo, ila pata picha enzi hizo 1987
Baada ya kukamilisha mpango wakachukua rooms Skyway hotel hapo posta, kwa ajili yao na watoto
4/
Keshowe ilikua siku ya bata kujipongeza, kisha siku inayofata Tohora, Sarah na watoto wakachukua ndege ya ATC kuelekea Kenya🇰🇪
Baada ya kufika Kenya wakachukua ndege nyingine kuunganisha Amsterdam hadi London.
UK🇬🇧 walikaa wiki nzima then wakachukua ndege kurudi Kenya
5/
By that time tayari huku TZ kilikua kimeshanuka, taarifa zilisambaa nchi nzima kuhusu ujambazi huo wa pesa nyingi sana.
Sarah na Tohora walikuwa ni most wanted wanatafutwa kila kona ya dunia
Wakiwa Kenya Sarah na Tohora wakaanza kununua assets, nyumba, magari na viwanja
6/
NBC tayari ilishamfukuza kazi Sarah kwa kutoonekana kazini kwa muda mrefu
Sasa, Trh 13/11/1987 Tohora akiwa office ya Toyota Nairobi akinunua gari, alijikuta yupo chini ya ulinzi
Wakambana aeleze alipo Sarah, Tohora hakuwa na option zaidi ya kuwapeleka maaskari alipo Sarah
7/
Kufika chumba 322 Jacaranda hotel- Nairobi, Sarah alikamatwa.
Serikali🇹🇿 ikatuma kwa serikali🇰🇪warranty ya Sarah na Tohora kurudishwa nchini kujibu mashtaka yao
Tohora alifanikiwa kukwepa extradition ila Sarah alirudishwa nchini na kukabidhiwa chini ya maafisa wa ulinzi
8/
10/2/1988 Sarah alifikishwa Kisutu chini ya ulinzi mkali. Mji wote ulijaa, barabara zilifungwa, watu waliacha kazi na kutoroka maofisini kuja kumuona huyo Sarah anafananaje
Ilikua ni kesi yenye msisimuko sana.
Sarah alikua anasimamiwa na Dr.Masumbuko Lamwai na alikiri makosa
9/
Baada ya kukiri makosa yote, Hakimu Mh. Masanche alitoa adhabu ya kifungo cha miaka 7 jela na kumuamuru Sara kurudisha pesa zote alizokwapua
Upande wa mashtaka haukuridhika na adhabu hiyo, kwamba ni ndogo haiendani na jinai aliyotenda Sarah, hivyo wakakata rufaa.
10/
Jaji Nassor Mzavas alisimamia rufaa hiyo, baada ya kusoma hukumu, Sarah alihukumiwa kifungo cha miaka 28 jela.
Sarah Simbaulanga alitumikia kifungo chake Keko, na sasa yupo nje. Sasa hivi ameamua kumrudia Mungu, ni mlokole yupo maeneo ya Kawe DSM
11/
Tukiwa tunaelekea siku ya wapendanao, Valentine's;
Usiruhusu penzi likucontrol, likudanganye, likusahaulishe wewe ni nani, malengo yako ni yapi, ukajisahau ukaacha kufanya majukumu yako kisa upendo.
Kumbuka riwaya ya Ngoswe Penzi kitovu cha uzembe.
Mwisho:

Loading suggestions...