SIR JEFF⚡🇹🇿
SIR JEFF⚡🇹🇿

@Sirjeff_D

21 Tweets 3 reads Jan 10, 2024
-Nimemaliza kusoma kitabu cha 2 kwa 2024
-Oliver Twist ni one of my favorite childhood novel
-Napenda sn Victorian🇬🇧 era books fiction sijui kwanini ila uandishi wa authors ni classic sn
-Oliver main character kapigika sn maskini ya Mungu tangu siku ya kwanza kuliona jua
UZI 🧵
1/
-Dogo Oliver ni km ana kimavi
-Kila janga linamkuta yeye.
-Picha linaanza anakosa mama, kuzaliwa kwake kidogo afe kwasababu ya mapafu kufail
-Mama yake anakufa akijifungua
-Analelewa kwenye kituo cha watoto yatima ambapo kuna mateso sn, kulimishwa, misosi mibovu
2/
Oliver ni dogo flani unatamani uingie kwenye kitabu, umkumbatie, umchum, umpe maneno ya busara
-Siku ya BD yake miaka 8 dogo kayatimba kwenda kuomba aongezewe uji bcs hajashiba
-Mr Bumble mzee mnoko kiongozi wa kituo cha Yatima akaona Oliver ni msumbufu akaamua amuuze kwa £5
3/
-Ilibaki kdg tu Oliver auzwe kwa mfanya usafi wa zizi la ng'ombe
-mwishoe akapigwa bei kwa undertaker, mzee wa misiba, mchonga majeneza, mchimba makaburi
-Yani dogo hana nyota kbs. Huko aliponunuliwa alibidi awe kijakazi, kusaidia mishe za majeneza na mazishi
4/
-Kwa undertaker⚰️ akakutana na jamaa flani jau sn anaitwa Noah na Dada wa kazi Charlotte nae ni Mavi Mavi tu. Wakawa wanamtesa sana Dogo Oliver
-Wanamnyima msosi, wanampiga, wanamlisha makombo, full manyanyaso
-Siku 1 Noah akamtukania mama yake ambae amekufa. Uchawi tu
5/
-Alivyodhihakiwa mamake Oliver akajam, akakinukisha, akampiga sn Noah kdg amuue
-Baada ya hilo soo, Oliver akaona bora atoroke
-Akatoroka, siku 7 dogo anapiga kwata akatafute maisha London.
-Kufika London kibahati akakutana na dogo mwngn wa age yake anaitwa Jack. Akampokea
6/
-Jack akampeleka kwa boss wake anaitwa Fagin, hapo at least Oliver akapata sehemu ya kupoa, kula na kuanza kutafuta life London
-Kumbe Fagin ni mtu wa michezo michafu aisee. Anawachukua mayatima na kuwafundisha kazi ya udokozi/pick pocketing. Kupiga doko km wahuni wa Kkoo
7/
-Oliver akafundishwa kazi ya kupiga doko. Mission ya Fagin akamwambia yy na kijana mwingine wakafanye udokozi
-Walivyoenda kuiba Oliver alikua anasoma mchezo unavyochezwa, mwenzie alivyomdokolea mzee mmoja watu wakashtuka
-Wakaanza kukimbizwa, bahati mbaya Oliver akakamatwa
8/
-Dogo alivyokamatwa akagongwa sn vitasa, ila pona pona yake akatetewa na mashuhuda walioona tukio Zima. Kwamba dogo hajaiba aliyeiba katoroka
-Mzee aliyeibiwa Mr. Brownlow mtu poa sn aise. Akamuonea huruma dogo akamchukua na kumpa hifadhi nyumbani kwake huku akimtibu
9/
-Dogo akawa na utawala na amani tele maana Mzee Brownlow alikua mtu poa sn
-Lile genge la uhalifu la Fagin wakawa na mashaka kuwa Oliver anaweza kuvujisha siri zao, so ikabidi msako uanze kumrudisha dogo kwenye genre
-Siku 1 dogo kaagizwa na mzee Brown aende mjini
10/
-Kufika town akakutana na sister mmoja muhuni tu anaitwa Nancy ambae ni demu wa jambazi anaitwa Bill Sykes ambae ni gang member wa Fagin
-Nancy akamrubuni Oliver kua anamjua na ni ndugu yake, dogo akajaa box, Nancy akafanikiwa kumrudisha bwana mdogo kwenye genge la wizi
11/
-Mission iliyofata Oliver akalazimishwa kwenda na jambazi Bill Sikes kufanya uhalifu kwenye nyumba ya bi'mkubwa mmoja anaitwa Maylies
-Dogo alitakiwa apenye dirishani aingie ndani afungue kitasa ili Bill Sikes akamilize mchongo
-Mlinzi akamuona dogo akapigwa shaba maskini🔫
12/
-Bahati nzuri dogo hakufa na Bill Sikes akatoroka eneo la tukio
-Bi'mkubwa Maylies aliyekuja kuvamiwa ana roho nyeupe kbs
-Akamchukua Oliver akawa anaishi kwake na binti mwingine anaitwa Rose ambae bimkubwa alim-adopt
-Dogo akawaeleza story yake yote wakaona wamsaidie
13/
-Dogo anahurumisha, maisha yake ni km digidigi, nuksi, mikosi, majanga,hajawahi kuwa na furaha
-Bimkubwa akamleta Dr. Losbern ili kumtibu jeraha la 🔫. Mdogo mdogo Oliver Twist akaanza kurejea kwenye afya yake, mwishoe akapona
-Hakuwa na furaha akijua wazoo Fagin anamtafuta
14/
-Fagin akaamuru msako uanze wa kumrudisha Oliver kwenye genge
-Akampa task kijn wake mmoja anaitwa Monks.
-Monks akafanya upelelezi kupitia Mr. Bumble yule mzee wa kituo cha kulea watoto yatima
-Monks Akamlipa Mr. Bumble & mkewe wampe siri 1 aliyoacha mama Oliver kabl kufa
15/
-Siri iliyofichika ni kubwa, ni mkufu aliouacha mama yake ukionyesha jina lake 'Agnes'
-Kumbe Agnes mamake Oliver alikua hawara wa tajir mkubwa anaitwa Leeford ambae alikufa kabla dogo kuzaliwa
-Kwenye urithi wake alisema nusu ya mali zake apewe mtoto atakayezaliwa na Agnes
16/
-Kumbe Monks nae ni mtoto wa Leeford so yeye na Oliver ni watoto wa baba mmoja, na hizo mali za urithi walitakiwa kushare 50/50
-Monks alivyo na tamaa alitaka dogo asipatikane identity yake ili yeye arithi kila kitu
-Dogo hn furaha, analia tu makaburini, anajua anatafutwa
17/
-Bimkubwa akaona ampeleke dogo sehemu salama, wakapanga safari bimkubwa, Oliver na Rose kwenda London.
-Rose akakutana London bridge na rafiki yake Nancy, yule demu wa Jambazi Bill Sikes aliyemtorosha Oliver kutoka kwa mshua Brownlow
-Nancy akachoma mpango wa Fagin na Monk
18/
-Taarifa kuwa Nancy amemsanua Rose kuwa Oliver anabidi auwawe zikamfikia mpenzi wake jambazi Bill Sikes.
-Bill Akaona km kasnichiwa, akampiga risasi Nancy na akafa hapo hapo, nae Bill akazidiwa ujanja baada ya kuuwa nae akajinyonga
19/
-Bimkubwa, Rose na Oliver wakafanikiwa kufika kwa mzee Brownlow. Kupitia siri alizovujisha Nancy yule aliyeuwawa baba wa Oliver akatambulika
-Kumbe pia baba wa Oliver alikua rafiki dam-dam wa mzee Brownlow na msimamizi wa mirathi
-Mzee akasimamia show hadi Dogo akapata haki
20/
-Genge la Fagin likadakwa na watu wa usalama likasambaratishwa love na Fagin akahukumiwa kifo
-Bimkubwa na Rose wakaenda kuishi kwa amani nje ya London, huku Oliver akiwa na utajiri mkubwa sn wa urithi akawa adopted na mzee Brownlow
-OLIVER TWIST akapata furaha ya kuishi

Loading suggestions...