Ndahani N. Mwenda
Ndahani N. Mwenda

@ndahani_mwenda

22 Tweets 63 reads Jan 05, 2024
UTT-AMIS ni kitu gani haswaa?
Ni kampuni ya uwekezaji/upatu?
Nikiwekeza pesa zangu kwao zitakuwa salama kwa kiasi gani labda kwamfano?
Nitapata faida kiasi gani nikiwekeza?
Kujua zaidi na zaidi, soma hapo chini!
#AskMwenda
UTT-AMIS ~ Unit Trust of Tanzania Asset Management & Investment Scheme, ndiyo kirefu chake!
Ni mfuko wa uwekezaji wa pamoja Tanzania. Na ndiyo mfuko wa kwanza wa uwekezaji nchini ambao mpaka sasa upo chini ya Wizara ya Fedha ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
#AskMwenda
Taasisi hiyo wakati inaanzishwa mwaka 2005, ilikuwa na mfuko mmoja wa UMOJA FUND ambao ulizinduliwa mwaka huohuo na kipande kimoja cha mfuko huo kiliuzwa TZS 100 tu.
Lakini leo 05 Jan 2024 kipande kile kile kilikuwa kinauzwa TZS 984.76 kikuwa ndiyo kipande ghali. #AskMwenda
Kufikia mnamo 05 Januari 2024!
UTT-AMIS ilikuwa na mifuko 6
~ Umoja Fund
~ Wekeza Maisha
~ Watoto Fund
~ Jikimu Fund
~ Liquid Fund
~ Bond Fund
#AskMwenda
Kufikia 31 Disemba, thamani ya mifuko yote kwa ujumla ilikuwa ni sawa kiasi cha zaidi ya TZS 1,000,000,000,000 huku MFUKO WA UKWASI (Liquid Fund) ukiwa na thamani ya juu kuliko yote ya zaidi TZS 890bln #AskMwenda
THAMANI YA MIFUKO 29 DIS 2023
a. UMOJA FUND
~TZS 339.98bn
b. WEKEZA MAISHA
~ TZS 12.06bn
c. WATOTO FUND
~ TZS 14.56bn
d. JIKIMU FUND
~TZS 22.99bn
e. LIQUID FUND
~ TZS 890.74bn
f. BOND FUND
~ TZS 542.09bn
#AskMwenda
UMOJA FUND ~ Ndiyo mfuko wa kaanza kuanzishwa na UTT mwaka 2005 taasisi hiyo ilipoanzishwa.
Sera yake ni kuwekeza chini ya 50% ya fedha za mfuko huo kwenye hisa na 50% kwenye hatifungani za serikali, za kampuni na FDR #AskMwenda
Kwenye huu mfuko..
~ Mtu binafsi, vikundi, taasisi zinaruhusiwa kuwekeza
~ Wawekezaji wa mfuko huu ni raia wa Jumuiya ya Afrika Mashariki pekee
~ Hakuna ada ya kujiunga
~ Kiwango cha chini cha kununua vipande ni 10 tu!
~ Utakatwa 1% wakati wa kujitoa
#AskMwenda
Kwenye Mfuko wa Umoja..
~ Vipande vinaweza kuhamishwa kutoka kwa mmiliki kwenda kwa mke/mme/watoto/rafiki
~ Mchakatao wa kununua na kuuza huchukua siku 10 za kazi
~ Vipande vinaweza rithiwa endapo mmiliki akifa
~ Vipande vinaweza tumika kama amana kuombea mkopo
#AskMwenda
WEKEZA MAISHA FUND, Ni mfuko wa pili wa UTT-AMIS uliasisi mwaka 2007.
~ Mfuko huu una faida kama vile Bima ya Maisha, Fidia ya Ulemavu
~ Pia fidia ya kifo endapo mmiliki atafariki, warithi watalipwa fidia
~ Huwezi weka kama amana ili upate mkopo taasisi ya fedha
#AskMwenda
Mfuko wa Wekeza Maisha...
~ 99.0% ya fedha zinawekezwa kwenye hisa, hatifungani nk
~ 1.0% ya fedha ni kwaajili ya Bima
~ Unaruhusiwa kuwekeza kwa miaka 10 tu ktk madirisha mawili
~ Ni kwaajili ya wawekezaji wanaokuza mtaji kwaajili ya baadae
#AskMwenda
Mfuko wa Wekeza Maisha...
~ 60% ya fedha zinawekezwa kwenye hisa
~ 40% kwenye hatifungani na FDR
~ Ni kwaajili ya watu wenye umri wa miaka 18-55
~ Uwekezaji wa vikundi haurusiwi
~ Utatozwa 2% utakapojitoa kabla ya 5yrs
~ Hakuna ada ya kujitoa baada ya 5yrs
#AskMwenda
WATOTO FUND, Ni mfuko maalum kwa kuandaa baadae njema kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka 18
~ Ulianzishwa mwaka 2008, ndiyo mfuko wa tatu kwa ukongwe pale UTT
~ Kima cha chini cha kuanza kuwekeza ni TZS 10k tu, na ukitaka kuendelea kuongeza uwekezaji ni TZS 5k
#AskMwenda
Mfuko wa Watoto...
~ Sera yake, 50% ya fedha zinawekezwa kwenye hisa na 50% kwenye hatifungani n FDR
~ Uwekezaji unaweza fanywa kwa jina la mtoto mwenyewe
~ Uwekezaji kama kikundi hauruhusiwi
~ Hakuna ada ya kujiunga
#AskMwenda
Mfuko wa Watoto...
~ Mtoto anaweza kukua nao mpaka atakapofikisha 24yrs
~ Ada ya kujitoa ni 1% kabla ya miaka 3 ya uwekezaji
~ Baada ya miaka 3 hakuna ada ya kujitoa
#AskMwenda
JIKIMU FUND, Ni mfuko wa 4 kuasisiwa na UTT-AMIS
~ Lengo la mfuko ni kukuza mtaji kwa wawekezaji
~ Mwekezaji akiamua kujitoa kabla ya miaka 3 ya uwekezaji anakatwa 1.5% ada ya kujitoa
~ Kima cha kuwekeza, TZS 2m kwa mara ya kwanza. Hutoa gawio baada ya miezi 3
#AskMwenda
Kwenye Mfuko wa Jikimu...
~ Unaruhusiwa kuendelea kuongeza uwekezaji kwanzia TZS 15k
~ Unaruhusiwa kuwekeza gawio/faida unayopata kwa kununua vipande
~ Ni maalum kwa watu wenye umri wa kwanzia miaka 18
#AskMwenda
MFUKO WA UKWASI, Ni mfuko ambao uwekezaji wake unahitaji pesa nyingi
~ Ni maalum kwa wawekezaji wanaotaka kukuza ukwasi wao
~ Sera ya mfuko huu 90% ya fedha huwekezwa kwenye hatifungani
~ Hatari ya kupoteza fedha ni mdogo
#AskMwenda
Mfuko wa Ukwasi...
~ Ni moja ya mifuko inayopendwa na wawekezaji wengi
~ Thamani ya mfuko ni zaidi ya TZS 890bn, ukiwa ndiyo mfuko wenye thamani kubwa kati ya mifuko yote
~ Ni maalum kwaajili ya kukuza ukwasi kwa ndani ya muda mfupi
#AskMwenda
BOND FUND, Kwa lugha nyingine unajulikana kama Mfuko wa Hatifungani
~ Ndiyo mfuko wa 6 wa UTT
~ Ulizinduliwa mwaka 2019
~ 90% ya fedha za mfuko huu huwekezwa kwenye hatifungani
#AskMwenda
Mfuko wa Hatifungani...
~ Kima cha chini cha kuwekeza katika mfuko huu ni TZS 50k
~ Kuna chaguo la kuwekeza kwaajili ya gawio, kuna gawio kila mwezi, 3 na miezi 6
~ Kwenye mwezi, utawekeza TZS 10m
~ Kwenye miezi 6, utawekeza TZS 5m
#AskMwenda
Mfuko wa Hatifungani...
~ Wawekezaji wa aina zote wanaruhusiwa
~ Kila mwezi mfuko huu hutoa gawio la TZS 1 kwa kila kipande kimoja
~ Kwa mwaka ni sawa na 12%
~ Ni mfuko mzuri kwa kukuza mtaji
#AskMwenda

Loading suggestions...