SIR JEFFโšก๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
SIR JEFFโšก๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ

@Sirjeff_D

18 Tweets 13 reads Jan 04, 2024
Kuna jamaa nilikutana nae huku bushi maeneo ya Ipogoro juzi trh 2 Jan. Ndani ya muda mfupi tu tuka-click vzr, tukaanza kupiga story za maisha.
Jamaa ni Msukuma wa Miswe anaitwa Nkulukulu, nae amekuja huku porini kujitafuta km mimi
UZI ๐Ÿงต๐Ÿ‘‡
1. Tangu nizaliwe sijawahi kusikia jina la Nkulukulu, so nikamuomba niwe namuita Nkulu. Nae hajawahi kusikia jina langu Sirjeff, akasema atakua ananiita SAA๐Ÿ˜„
Jamaa yuko mid 30s kwa kumwangalia japo sikumuuliza. Bahati mbaya hakufanikiwa kufaulu form4, alizungusha donut ๐Ÿฉ
2. Huo ukawa mwisho wa masomo yake. Basi Nkulu akaja Dar kutafuta maisha. Akakaa kwa mjomba ake miezi mitatu, akapata mchongo wa kuwa mlinzi kwenye Go Down huko kigamboni.
Nkulu ananiambia alikua analipwa 80K per month. Akapiga mishe kwa unoko sn, lkn baada ya mwaka hkn kitu
3. Mshahara wote unaisha kabla ya tarehe 20. Akaamua atafute sehemu nyingine ya kazi.
Kwasababu ana uzoefu akapata mchongo kwenye security company kubwa
Hapo Nkulu tyr nimempa utawala wote afunguke, hanijui vzr basi ananichukulia kinyonge sn, anajisifia anajua sn kupiga shabaha
4. Akapangwa kufany kazi ya ulinzi hoteli moja kubwa sana Posta, Dar.
Mshahara wake uliongezeka from 80K to 120K. Akapiga unoko sn hapo kwa miaka mi4.
Jamaa ni mtu mpole sn, mkarimu na mstaarabu sn, anasema alikua anapata sn vi-tip vya wateja, anajazilizia kwenye kibbutz chake
5. Hapo hapo hotelini akapata dem msaidizi wa mpishi, kwahiyo alikua anapata makombo, ukoko & mabaki ya misosi, so chakula haikua shida kwake
Miaka miwili baada ya kupiga unaa mwingi mshahara wa Nkulu ukapanda hadi 140K
Nkulu yy alikua na malengo yake tofauti, sio kua security
6. Nkulu alikua anasave pesa nia yake aingie kwenye kilimo. Mpk anaacha kazi after solid 4 yrs alikuwa na savings around 1,400,000
Akaongea na mjomba ake kuwa anarudi Miswe kujitafuta, anko ake akamuongezea laki5. Dem wake nae akamboost 200K ila alimuacha Dar, pale pale hotelini
7. Nkulu alivyorudi Miswe hakuelewa ramani kbs. Ananiambia alikua na rafiki yake BF anaitwa Mgendwa, walisoma Olevel pa1, ila yy alikua Muhehe.
Mgendwa akamshawishi Nkulu as a true friend km anataka kilimo aje kujitafuta Mufindi, Iringa.
Ndio Nkulu akaja Mufindi 2017 kujitafuta
8. Akapokewa na rafiki yake Mgendwa ambae yeye ni dalali wa viazi - hivi viazi mviringo vya chips
Nkulu na Mgendwa wakawa wanaenda pa1 kufanya ulanguzi wa viazi kutoka kwa wakulima kuleta town kuviuza
Ila Nkulu hakupenda hiyo mbishe, yy passion yake ni kilimo sio udalali.
9. Nkulu alikua na hela kiasi mkononi, akatafuta shamba Ipogolo - tulipokutana juzi.
Kuna shamba Nkulu akakodi heka 3 kwa Mmama-mjane. Huyo mama mumewe alifariki kwa njia za ajabu ajabu, mkewe akarithi maeneo
Ilo hlo shamba lina mgogoro: ndg wa mume wanasema ndugu yao aliuwawa
10. Nkulu hakujali hayo makelele kuwa shamba lina mgogoro. Baada ya muda akaanza kuandaa shamba ili aanze kulima viazi.
Siku moja wakaja bibi wawili na babu mmoja, wakamzingua sn Nkulu na kumchimba mkwara mnene kuwa asilime kwenye eneo lao. Hao wazee walikua ndg wa marehemu
11. Wakamwambia Nkulu kua asipisikiliza ama zake, ama zao. Hatovuna kitu na atajilaumu sana.
Haha hapo nikakumbuka 2015/16 nikiwa chuo nilivyoenda Mlimba kulima mpunga, ktk heka 45 nikavuna gunia 12. Baadae wazee wa kijiji wakaniambia "sikusalimia watu vzr, so wakanishughulikia
12. Kumbe Nkulu nae hajakaa kinyonge, baada ya vitisho vya wale wazee wa marehemu, yy akaendelea kuandaa shamba
Alivyomaliza akarudi Miswe. Yeye ananiambia alienda kwa Fundi wa kisukuma. Hatishiki na mtu yyt kiroho kwenye utafutaji.
Ananiambia "Nilipikwa Nyanda siku 3"๐Ÿ˜„
16. Mimi namsikiliza tu Nkulu. Kimoyo moyo simwelewu kbs, mm nimelelewa kidin, yani hivyo vitu ni dhambi mbaya sn.
Nkulu akarudi Mpogolo after 3 days, akaanza kilimo cha viazi. Akajenga kambi, akapanda mbegu, akatia ndagu za mganga, akapiga mishe kinoko akiwa ameajiri vijana wa3
17. Baada ya miezi 4 Nkulu akavuna viazi kibabe sana, heka 1 alitoa wastani wa gunia 38 na aliuza gunia 1 kwa sh 45,000 shambani,
Kwa heka zote 3 alipiga km mil 5, yy gharama zake zilikua kama 1.8, bcs alilima kienyeji. Hkn tractor, hakuna kupiga hallow, mbolea kapiga mara 1 tu
18. Nkulu ananiambia kila akiingia shambani lazima aende kwanza Usukumani kwa FUNDI wake.
Sasa hivi nimekutana nae ana heka zake 60 zaviazi, kwa huku ni Don mkubwa. Ana nyumba yake, ana guest house, ana Kigali kimoja na tractor ya mkopo, ana mpesa wakala na duka la nafaka
19. Mimi nna mpango nilime kiazi heka 20, lkn itakua pilot experiment, nia yangu niuze Dar - Mabibo sio huku Iringa.
Mjini kuazi kinatembea 100K hadi 120K. Huku zaidi wanalima mbegu ya Kidinya, ila mimi nataka nipige heka10 Kidinya, heka 10 Obama.
Lkn nina swali moja...
Hivi ni kweli Nkulu kafanikiwa kwa kutumia UCHAWI? Mimi siamini huo us* wa Fundi?
Any opinions?

Loading suggestions...