(---) Onesmo Mushi
(---) Onesmo Mushi

@EduTalkTz

4 Tweets 9 reads Mar 07, 2023
Elimu:
Rousseau ametusema sana wazazi kwenye hiki kitabu. Amesema miaka 7 ya mwanzo ndio inajenga msingi wa elimu lakini imejawa na neglect. Amewasema wanawake kwa kupuuzia kunyonyesha na kuwaachia wasichana wa kazi (kwa lugha ya kitanzania). Amesema haya kwa uchungu sana⬇️
Ametusema wanaume kwa kutokujali malezi na makuzi ya watoto wetu pale mwanzo. Amesema tunapuuzia malezi ya watoto na kuwafanya magarasha kisha after 7 years tunawapeleka shule tukitegemea walimu watende muujiza. Ametusema kwa kupeleka watoto wadogo boarding schools!⬇️
Rousseau ametusema kwa kuwanyima watoto kucheza na kuwaibia utoto wao. Ametusema kwa overparenting, amesema tunawapamper watoto sana kiasi kwamba wanashindwa kujifunza namna ya kuuishi uhalisia wa Dunia. Ametusema kwa mapenzi yetu kwa watoto yanayozidi mpaka kuwaharibu⬇️
Rousseau amesema elimu ya kwanza ni kumfundisha mtoto kuwa mtu, “training a kid to be a man,” na mwalimu pekee anayeweza kulifanikisha hili ni mzazi. Amesema wazazi tukilikoroga hapa mwanzo, tunaharibu Kabisa mpangilio wa elimu ya mtoto. Amesema tuwajibike, tucheze Nafasi zetu.

Loading suggestions...