Mwaka 2017, nikiwa nimeadhibiwa vizuri na maisha, nilisikia ile Warsha ya “Fursa, Anzia Sokoni” inakuja Morogoro. Nilikuwa nimeshajikatia tamaa kabisa ila kuna kitu moyoni kikaniambia “jaribu kukutana na Ruge Mutahaba umwombe ushauri, ameshasaidia vijana wengi kama ww”⬇️
#Thread
#Thread
Nilianza kustrategize namna ya kukutana na Ruge. Kama mnavyojua, jamaa alikuwa mtu mkubwa na maarufu sana kiasi kwamba ni vigumu kwa mtu wa kawaida kama mwalimu wa sekondari kukutana naye. Tena ilikuwa ngumu zaidi kwa siku ya Warsha ambayo alizungukwa na maelfu ya watu⬇️
Nilishare hili wazo na baadhi ya walimu wenzangu tuliokuwa tunajiita “WAMANTA.” Hata hivyo walimu wenzangu hawakuona uwezekano wa kulifanikisha hili. Walihisi kama naota; “wewe Onesmo wewe, unafikiri Ruge ni kama Mkuu wa shule unamsogelea tu?” mwalimu mmoja aliniambia.⬇️
Kama walivyosema walimu wenzangu, haikuwa rahisi katika fikra za kawaida kwa Mimi/sisi kukutana na Ruge siku ile. Tena tuliposikia ataambatana na Naibu Spika, @TuliaAckson , Mkuu wa Mkoa, wasanii maarufu kama Mrisho Mpoto pamoja na kundi zima la Clouds Media tukakata tamaa kbs⬇️
Hata hivyo ndani yangu bado niliamini inawezekana. Msukumo uliokuwa ndani yangu ulikuwa mkubwa na wenye nguvu kuliko udogo na uduni ulioonekana nje ya mwili wangu. Baada ya kuziamini fikra zangu, niliamua moja “NITAFANYA LOLOTE NDANI YA UWEZO WANGU NIKUTANE NA RUGE. NO PLAN B.”⬇️
Mungu ametuumba katika style ya ajabu sana. Fikra zako ukishazielekeza kwenye kitu kimoja na kuzilazimisha kwamba ni lazima zikifanikishe, aisee zitafanya kazi usiku na mchana, ukiwa macho na ukiwa umelala mpaka zikipatie majibu. Ndicho kilichotokea kwangu. ⬇️
Baada ya kuwaza namna nyingi hatimaye fikra zilinipa majibu. Kwanza ziliniaminisha kwamba inawezekana kukutana na Ruge kisha zikanipa mbinu na ujasiri wa kufanya hivyo. Mbinu ya kwanza ilikuwa kuwahi mapema ukumbini na kukaa siti za mbele, na pili ni kuhakikisha nawaza moja tu⬇️
Siku ya Warsha ya “Fursa, Anzia Sokoni” ilipowadia, nilikuwa miongoni mwa watu wa mwanzo kabisa kufika pale Nashera Hotel. Bahati nzuri hapakuwa na kiingilio. Masaa kama matatu kabla ya tukio, tayari Nilikuwa nimeshajiposition seat za mbele Kabisa na tena mwanzo karibu na njia⬇️
Plan yangu ilikuwa moja tu, Warsha itakapomalizika, haraka na kwa speed ya ajabu natakiwa kusimama na kukimbia stejini alipokaa Ruge kisha kumuomba angalau dakika chache za kuongea na Mimi. Niliamini kwamba kwa ule ughafla, asingeweza kunikatalia mbele za watu.⬇️
Nilijua kutakuwa na watu wengi wanaotamani kumsogelea na wengine wakitamani kupiga naye picha. Nilifahamu pia kuwa kutakuwa na vyombo vingi vya habari, wapambe watakaomzuia kukutana na Huyu na yule, lakini pia uharaka wa ratiba inayofuata. TIMING and EXECUTION were everything. ⬇️
Wakati Warsha inaendelea, fikra na akili zangu zilikuwa kwenye 1 tu, “wanasema neno la mwisho saa ngapi,” nilikuwa makini sana na Hilo. Warsha ikaendelea, mwishoni Ruge alipomalizia kutoa nasaha za mwisho tu, kwa kufuata instinct bila kufikiri mara mbili tayari nilishamfikia!⬇️
Yes, nilikuwa na hofu kubwa na adrenaline rash ya kutosha. Fasta baada ya kumsalimia, nikamwomba kwa sauti na hisia genuine kuliko kawaida, “kaka Ruge, tafadhali nakuomba angalau kwa dakika 10 tu. Sihitaji fedha wala kazi wala connection, nahitaji ushauri tu, please.”⬇️
Ruge aliniangalia na uduni wangu lakini naamini aliappreciate ujasiri niliouonesha na kuamini kwamba ombi langu lilikuwa genuine. Kisha akasema “dah, aisee wewe. Sasa fanya hivi, hapa kila mtu atataka kuongea na Mimi na kupiga picha. Nenda kanisubiri pale reception, usiondoke.”⬇️
Ruge alisisitiza kwamba Kuna uwezekano akachelewa kuja aliponiambia nimsubiri lakini niamini kwamba hajanisahau na atakuja. Nilienda pale reception na walimu wenzangu walioshindwa hata kuingia ukumbini. Tulimsubiri kwa Karibu masaa matatu and finally, he came. ⬇️
Long story short, ushauri binafsi alionipa Ruge siku ile baada ya kumwambia ninaichukia kazi ya ualimu niliyokuwa naifanya kwa wakati ule ndio uliosababisha nikahustle kupata ninachokifanya sasa. Aliniambia “ukiichukia kazi yako, itakufanya maskini. Ipende ili ikubadilishe.”⬇️
Mwaka 2019 nikiwa masomoni China, nilipata taarifa za kifo chake. Niliumia sana ila hapakuwa na la kufanya. Nilimshukuru kwa kugusa maisha yangu kwa zile dakika cha chache alizokubali kunishauri. Kwa kumbukumbu, nilinunua suti (DP) ya rangi aliyokuwa ameivaa siku ananishauri.⬇️
Moral of the story: Kuna watu wanatafuta mtaji, wengine connections, wengine maarifa, wengine power. Lakini pia Kuna watu wanahitaji ushauri tu kutoka kwa mtu fulani. Just trust your instinct, kijue unachokihitaji kisha kifanyie kazi kwa uaminifu.
#RIP #RugeMutahaba
#RIP #RugeMutahaba
جاري تحميل الاقتراحات...