Ndahani N. Mwenda
Ndahani N. Mwenda

@ndahani_mwenda

4 Tweets 39 reads Feb 24, 2023
24 Feb 2021 niliweka oda ya hisa 10k za CRDB kwa TZS 200/hisa.
Baada ya siku chache zikapanda hadi TZS 215/- SIKUNUNUA!
TZS 2m yangu ikarejeshwa kwenye akaunti, sijui hata nilifanyia nini LAKINI sasa hisa ileile inauzwa TZS 445. Unaona fursa niliyopoteza wakati huo? #AskMwenda
Kama ningenunua kwa TZS 215/- maana yake ningepata hisa 9,302 ambapo kwa leo ningesema niuze kwa TZS 445 ningepata TZS 4.139m faida ya TZS 2.139m sawa na 107%.
Ongezeko la Mtaji ni moja ya faida ktk uwekezaji wa hisa ambapo unanunua hisa kwa bei ya chini na kuuza kwa bei juu.
Unapotaka kuwekeza unahitaji uamuzi wa Kijasiri kwaajili ya manufaa ya baadae.
Baada ya kosa hilo sijawahi tena jiuliza mara 2x kwenye suala la kuwekeza. Kila napopata pesa wazo la kwanza huwa nikununua hisa.
Mnamo Disemba 2019 hisa moja ya CRDB iliuzwa TZS 95/- tu. Unadhani mtu ambaye alinunua walau hisa za TZS 5,000,000 tu leo mtaji umeongezeka kwa kiasi gani?
Je, vipi akiamua kuuza kwa bei ya sasa ya TZS 445/-? Faida yake ni karibia mara 4 ya alichowekeza.

Loading suggestions...