Tofauti kati ya hisa na hatifungani.
HISA - Ni sehemu ya umiliki wa biashara/kampuni. Unaponunua hisa za kampuni unakuwa ni mmoja ya wamiliki wa hiyo kampuni husika.
HATIFUNGANI - Ni mkopo ambao Serikali/Kampuni huingia makubaliano na mtu, taasisi ama mashirika! #AskMwenda

Ukinunua hisa unakuwa mmoja ya wamiliki wa kampuni na hivyo una haki mbalimbali hata kama unazo hisa kidogo. Haki hizo ni pamoja na kupata gawio, kuhudhuria mkutano mkuu na zinginezo nyingi.
Unaponunua hatifungani unakuwa umeikopesha Serikali/Kampuni na muda ukiisha wa makubaliano wanakurejeshea pesa zako.
Hata kampuni ikifilisika ni lazima wakulipe kwa kuuza mali zao maana hilo ni deni tofauti na hisa.
Serikali ikifilisika ni ngumu kukulipa pesa zako ulizowekeza.
Hata kampuni ikifilisika ni lazima wakulipe kwa kuuza mali zao maana hilo ni deni tofauti na hisa.
Serikali ikifilisika ni ngumu kukulipa pesa zako ulizowekeza.
Zipo aina nyingi za hatifungani, Kuna hatifungani za serikali (Treasury Bonds) na zile za makampuni (Corporate Bonds) lakini pia zipo za Manispaa (Municipal Bonds) na zingine nyingi ikitegemea na mtoaji na lengo pia.
Kuna hatifungani za miundombinu, hatifungani za vita nk!
Kuna hatifungani za miundombinu, hatifungani za vita nk!
Pia zipo aina nyingi za hisa kama vile hisa za kawaida (Ordinary Shares) , hisa za upendeleo (Preferred Shares) pia kuna hisa za kampuni (Corporate Shares) na zinginezo nyingi.
Loading suggestions...