nikki_wa111
nikki_wa111

@NikkiWa111

22 تغريدة 4 قراءة Mar 17, 2024
JALADA #5: - THREAD -
YASIYOSEMWA KIFO CHA MAGUFULI, CDF MABEYO KIKWAZO, FISI WALIITAMANI MAGOGONI!
Unakumbuka tarehe 17.03.2021 Makamu wa Rais (wakati huo) SSH anatoa taarifa ya kifo cha Rais Magufuli?
Uliona nini kwenye sura yake?.....
#Tushuke.
'CHRONIC ATRIAL FIBRILLATION (AFiB)
Tuanze na tangazo la Mama SSH kuwa JPM amefariki kwa tatizo la mfumo wa umeme wa moyo, kifupi (AFiB).
Tatizo hili husababisha moyo kushindwa ku-control mapigo, hivyo mapigo yanaweza kushuka sana (mpaka 40) au kwenda kasi isivyo kawaida.
Kwa muda gani #JPM alikuwa na AFiB?
Kwa taarifa ya kifo, kauli inayotoka kwa Mama #SSH ni kwamba #JPM amekuwa na #AFiB kwa miaka 10.
Turudi nyuma: Miaka 10 nyuma ya 2021, maana yake #JPM amekuwa mgonjwa tangu 2011 au zaidi.
AFiB & Stroke ni Mti na Mtunda wake!
Dalili & madhara ya tatizo la umeme wa moyo ni pamoja kuchoka sana, kukosa hewa na kupata stroke sababu mirija ya damu haipati msukumo wa kutosha hivyo damu inaweza kuganda katikati ya mishipa ika-block flow ya damu mwilini haswa kichwani.
TIBA YA TATIZO LA UMEME WA MOYO
Tiba kuu ya AFiB ni kufungwa betri za moyo (Pacemaker) kifuani. Hii mashine inadhibiti mapigo ya moyo kutoshuka sana au kupanda sana sababu umeme wa moyo tuliopewa na Mungu hauwezi tena jukumu hilo.
Tazama picha hapa chini.
MAGUFULI ALIPELEKWA JKCI KIMKAKATI
JKCI waliwezeshwa mtambo aa kuweza kupandikiza betri kifuani (Pacemaker) tangu 2019.
Mkurgenzi wa Tiba ya Moyo JKCI (wakati huo) Dr. Peter Kisenge alifanya kipindi maalum kuzungumzia mtambo huo mpya mwezi Machi, 2020.
MAGUFULI ANUNUA MASHINE YA KUDHIBITI MAPIGO YA MOYO KWA BIL 4.5 JKCI
Dr. Kisenge (Video chini) Machi 2020, jitihada za serikali kununua mtambo ambao unapachika betri (Pacemaker) kwa wagonjwa wa tatizo la umeme wa moyo. (AFiB)
N.B: #JPM ni mhanga wa tatizo hilo wakati huo wote!
Nini hutokea #Pacemaker ikifeli?
Betrii inapofeli, asilimia za kupata stroke huongezeka mara tano zaidi na hatari ya kifo kutokana na cardiac arrest huongezeka zaidi.
Hii hutokana na mapigo ya moyo kutokuaa under control tena.
Chronic AFiB maana yake inaweza last hata wiki+
UANAJESHI WA CDF MABEYO KAZINI!
Baada ya kuufahamu ugonjwa, turudi kwenye statement za CDF Mabeyo.
"Mzena tuli-limit watu ili apate kupumzika vizuri" -CDF
Kiuhalisia ni kwamba ilifanyika security upgrade kwa Hayati #JPM sababu Mzena ulinzi ni wa hali ya juu kuliko JKCI.
MABEYO ACHEZA KI-KOMANDO!
Ikiwa JPM alinunua mashine ya tatizo la umeme wa moyo kwa Tshs. Bil 4.5 JKCI, akapelekwa hapo kutibiwa tangu Machi 06 na ikiwa JKCI ina V.I.P wards, ilikuaje ashindwe kupumzika vizuri mpaka ahamishwe Mzena?
Maana yake CDF aliamua kurudi ngome!
TULIKUWA WATATU, WAKATI #JPM ANAKUTWA NA MAUTI.
CDF, IGP & DGIS walikuwepo wakati Amiri Jeshi Mkuu (wakati huo) anaaga dunia.
CDF kama Mwenyekiti wa wakuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama anaamua kuchagua KATIBA inasemaje!
Inaleta MAJADILIANO kadhaa....
PM MAJALIWA & KMK BASHIRU WAITWA MZENA, MAMA YUKO TANGA.
Kutoka Dodoma, KMK anakuja Daslaam bila kujua habari za msiba.
Dar - Dom = Masaa 7 kwa gari.
Dar - Tanga = Masaa 5 kwa gari.
Katiba inaelekeza Makamu aapishwe kuwa Rais ndani ya masaa 24.
MAMA ANAPEWA TAARIFA, ATANGAZE MSIBA!
Akiwa Tanga, anahutubia kupitia TBC kuwa Rais Magufuli amefariki na alilazwa tangu Machi 6.
Ukimtazama sura ya #Mama wakati anahutubia, unajiuliza maswali mengi.
Ni lini alifahamu taarifa hiyo....
AFiB inajulikana, pacemaker ikifeli.
MAMA ZIARANI TANGA, NA JIOGRAFIA YA TANGA
Njia ya kuingia Tanga na kutoka ni moja pekee kwa level ya msafara wa ngazi ya U-Rais.
Kiulinzi, ni rahisi kumzuia mtu asiingie wala kutoka Tanga kuja mikoa mingine ukidhibiti njia kuu (Inlet & Outlet) pamoja na bahari.
TIMING YA KUTANGAZA MSIBA, CDF MABEYO KIKWAZO!
Kutangaza msiba haraka, ingeharibu mipango yoyote ya kujaribu kwenda kinyuma cha Katiba kwa mtu yoyote.
CDF kama M/Kiti wa Usalama, alibeba jukumu la kutoa taarifa kwa Mama akiwa Tanga kukagua miradi ya maendeleo.
CDF NA ULINZI KWA RAIS SAMIA TANGA
Mkuu wa Majeshi, anawajibika moja kwa moja, na ulinzi wa Rais-Mtarajiwa.
Jeshini hakunaga ku-assume suala la ulinzi.
#SSH akiwa Rais Mtarajiwa (kabla hajaapishwa) ulinzi wake unaimarishwa zaidi na CDF.
CDF Mabeyo adressed the matter!
KATIBA INASEMAJE RAIS ANAPOFARIKI MADARAKANI?
Ibara ya 37(5) inaelekeza Makamu wa Rais ndie aapishwe kuwa Rais mara moja.
IKITOKEA MAKAMU WA RAIS HAYUPO, NANI ANGESHIKA NCHI?
Hapa ndipo kwenye vurugu na mtego mkubwa!
Katiba inasema, iwapo Makamu wa Rais hayupo, basi mamlaka ya nchi yatakasimiwa kwa SPIKA WA BUNGE LA JMT.
Ambapo baada ya muda ataitisha uchaguzi mkuu wa nchi.
Maswali ya kujiuliza:
Ni mazingira gani Makamu wa Rais angeweza kuwa hayupo?
Nani alipanga ziara ya Tanga?
Kwanini majadiliano yalikuwa mengi mpaka Mama kuapishwa!
Je, kulikuwa na harufu yoyote watu walichungulia kiti cha Magogoni wakaona wamekikaribia?
MABEYO ATOA AMRI SAMIA AAPISHWE KWA GWARIDE MAALUM:
Wakati wengine wakishauri asifanyiwe sherehe ya uapisho kwa gwaride wala bendera, maana yake Jeshi lisingemtambua kama Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama.
Hii ina maana, asingekua na mamlaka ya kuamuru majeshi!
KUZALIWA KWA AWAMU YA 06.
Baada ya bendera ya Rais aliyefariki kushushwa, ikapandishwa bendera ya Rais wa sasa, SSH.
Hii ikiashiria awamu ya tano imeisha sasa ni awamu ya 06, chini ya Amiri Jeshi Mkuu mpya.
Hivyo vikosi vyote vinapokea amri kutoka kwa Amiri Jeshi mpya.
- FINAL -
Nchi imepata mfano bora, wa askari na afisa wa Jeshi (4 Star General) ambae anaishi kiapo chake na kufa akiwa Mwanajeshi katikati ya wimbi ambalo angeweza kujiokotea dodo lolote!
Tanzania itamsoma katika vitabu vya mafunzo, huko baadae!
SALUTE!

جاري تحميل الاقتراحات...