13 Tweets 2 reads Feb 20, 2024
Mambo MUHIMU kabla haujaanza kujihusisha na FOREX. Uzi wote uko hapa chini 👇 #riplowassa pray for congo
Mambo vipi?! wananiita Infinity, nataka nikuchukue hatua moja mpaka nyingine, hadi utakapoona unaweza kutembea mwenyewe kwenye hii biashara inayoenda kwa jina la FOREX.
Tutatumia lugha ya kiswahili kwa sababu tangu nipo shule hii ndio ilikua lugha yangu, na majina ya “swahili speakers” yalikua yananihusu saana hahahaha!!!
Sasa kabla hatujaanza kujifunza hii biashara, kuna mambo ya muhimu ambayo inabidi uyazingatie sana ili usije ukakwama au ukaona mambo ni magumu kwa namna moja ama nyingine, haya hapa chini;
1.Vifaa:   Unahitajika kuwa na kompyuta, iwe desktop au laptop, uwe na simu janja (smart phone) ukikosa kimojawapo kati ya kompyuta au simu janja usijali, umeme usiokua wa kusuasua pamoja na mtandao mzuri wa internet, kwani hii biashara inafanyika moja kwa moja mtandaoni.
2.Muda:   Muda ni kitu kikubwa sana katika biashara hii, kwani yawezekana kabisa ndio ikawa biashara pekee ya maisha yako, unahitaji muda wa kutosha kufanya mazoezi, vilevile unahitaji muda wa kutosha kujifunza,na kusoma baadhi ya vitabu.
3.Dhamira/ Nia:   Skia, hakuna njia rahisi ya kutengeneza pesa! kama uliamua kuitafuta FOREX baada ya kuskia mtu flani kawa tajiri ndani ya muda mfupi, ni bora uache tu ukaendelee na mambo mengine hata kuskiliza mziki!! FOREX inahitaji uvumilivu, kuna wakati utaona kama huelewi,
muda mwingine unaona umeelewa lakini kila order ukiweka inaenda kinyume na wewe, utachoma account kadhaa, hapo ndipo ujue umekaribia kua fundi, komaaaaa!!!!
vilevile upunguze ulafi!!! wakati huu ni wa wewe kujifunza na kulizoea soko, sio wakati wa wewe kutengeneza pesa ndefu ya kukufanya uache kazi uwe unalala ndani tu. kwahiyo usitegemee kutengeneza pesa ndefu ndani ya huu muda mfupi, jifunze kwanza kisha mengine yatafuata.
Unaambiwa ni 5% tu ya watu wanaojifunza Forex ndio hufanikiwa, 95% huwa wanashindwa! sababu kubwa hua ni elimu mbovu (ukiwa hapa utapata elimu tamu), tamaa, ulafi, na kukosa uvumilivu. Jiepushe navyo kabisa.!!!
4.USIOGOPE!!!    Kama umeweza kuifikia hii sentensi basi wewe una asilimia nyingi za kufanikiwa!!! wenzio baada ya kuona hivyo vikwazo hapo juu hawakusubiri kufika mwisho, wamekata wakaendelea na mambo mengine hahaha!!
kama wewe umefanikiwa kufika hapa basi na mie nitajitolea kwa nguvu zangu, akili, muda, na kila kitu kuhakikishia nakupa ufundi wa kutosha ili uweze kutengeneza pesa. Zingatia tu ulichokisoma hapo juu na kila kitu kitaenda sawa.
Kwa sasa tuishie hapa, nasubiri maoni na maswali yako hapo chini, usisahau kurepost na kulike na wenzio wapate haya maarifa,ili wote tufaidi. Tukutane hapo mbele kwa somo la FOREX NI NINI???!!! Link ya Darasa kwenye bio yangu. Bureee!!

Loading suggestions...