Binti huyu (marehemu) anatokea familia ambayo inajiweza, isitoshe alikua mfanyakazi katika taasisi moja (jina nalihifadhi) akiwa ni binti ambae tayari alikuwa na hatua ya kuwa na usafiri binafsi pamoja na nyumba yake ya makazi, pia familia yake ni familia ambayo haina shida.
Hivyo comment za watu, kuwa ilikuwaje akaolewa na Koplo wa kaki, wakisema kuwa ni umasikini, hapana....hapo mmemuonea bure, binti alimkataa mwanaume mwenye maisha ya zaidi yake, mazuri na kila kitu kwa sababu anazozijua yeye mpaka leo amelala mauti, kaburi pekee ndilo linajua.
Marehemu alikuja kuolewa na Koplo Aron. J.
Ndoa ilikua salama, na Koplo yule alikua akitumia usafiri wa mke wake, (yaani gari moja) sababu marehemu alikuwa na gari mbili.
Wakafanikiwa kupata mtoto mmoja, ambae kwa nafasi kubwa mtoto huyu alilelewa sana na mdogo wa marehemu..

Mdogo wa marehemu (akiwa chuo) ndie alieshiriki kwa nafasi kubwa malezi ya mtoto huyo, kwani wazazi wawili wote walikuwa bize na kazi, na pia kutokana na kufanana kwa marehemu na mdogowe, ilifika hatua mtoto alikuwa akimuita mama mdogo kama "Mama".
Turudi kwenye kisa halisi sasa
Turudi kwenye kisa halisi sasa
Mwaka 2023 ni mwaka ambao familia ya marehemu ilimpoteza marehemu (binti yao) pamoja na Mama yao mzazi ndani ya kipindi cha mwezi mmoja wa vurugu na kashikashi za msiba, mivutano na polisi, kukimbizana maporini & kushinda hospitali.
Familia mpaka imeamua kutoka kwenye jamii kuomba msaada wa kisheria na ki-njagu, ni baada ya kukosa ushirikiano kwenye kile inachohisi ni kifo cha binti yao hakikuwa cha ugonjwa wa kawaida kwa ushahidi wa kimazingira wakiunganisha dots za jinsi mume wa marehemu alivyofanya...
Ndoa ya binti yao ilianza kuwa na migogoro isiyoisha haswa marehemu akilalamika juu ya vitendo vya imani za kishirikina vya mumewe huku akijitetea kuwa anafanya hivyo ili apande cheo kazini pia inasemekana mumewe aliingia mahusiano na mmoja wa askari wa kike mwenye cheo kikubwa.
Hapa sasa, picha inaanza kuja ni kwa vipi familia ya marehemu iliweza kudhibitiwa hospitali na pia kwenye mazishi ya marehemu kuwekewa ulinzi full na familia ya marehemu ikiwemo baba wa marehemu kuwekwa chini ya ulinzi kiasi hawakuruhusiwa kuaga mwili wa binti yao.
Familia ina mashaka kuwa siku ya kifo cha marehemu, marehemu alikua mzima wa afya, na alionana na nduguze asubuhi yake akiwa mzima majira ya asubuhi na hata kuongea nao kwenye simu wengine. Taarifa ya kifo cha marehemu wamekuja kuambiwa akiwa tayari ni maiti hospitali mchana.
Siku ya kifo cha marehemu, mumewe alimletea chakula cha mchana kutoka katika mgahawa, alimuomba watoke baada ya kugombana usiku wa jana yake, hivyo walivyofika njiani akaenda mletea chakula na kumletea kwenye gari. (Hawakwenda wote mgahawani, alimletea chakula kwenye gari)
Baada ya kula chakula kile, ndipo hali ya marehemu ikabadilika na kuanza kulalamika.
Mumewe (Cpl. Aron) akamkimbiza hospitali Hindu Mandal.
Inachotia mashaka ni, katika hii process yote, Cpl. Aron hakutoa taarifa kwa yoyote hata kwa mdogo wa marehemu ambae yuko karibu na familia
Mumewe (Cpl. Aron) akamkimbiza hospitali Hindu Mandal.
Inachotia mashaka ni, katika hii process yote, Cpl. Aron hakutoa taarifa kwa yoyote hata kwa mdogo wa marehemu ambae yuko karibu na familia
Taarifa kwa familia ya marehemu kuhusu kifo cha binti yao, imekuja kuwafikia ikiwa tayari binti amelala mauti.
Hiyo ni upande mmoja, upande mwingine ni mazingira ya kuuhamisha mwili Hindu Mandal kuupeleka Hospital ya manjagu Kurasini.
Hiyo ni upande mmoja, upande mwingine ni mazingira ya kuuhamisha mwili Hindu Mandal kuupeleka Hospital ya manjagu Kurasini.
Mwili wa marehemu tangu ukiwa Hindu Mandal mpaka unafika Hospital ya Polisi, hakuna ndugu yoyote wa upande wa marehemu aliyeuona wala kuutambua. (HAWAKURUHUSIWA) na kuliwekwa ulinzi mkali wa manjagu.
Ni kwanini haya yote yanafanyika? Inatia mashaka sana!
Kinafichwa kitu gani?
Ni kwanini haya yote yanafanyika? Inatia mashaka sana!
Kinafichwa kitu gani?
Muda wote ambao mwili wa marehemu umehifadhiwa hospital ya manjagu, walioruhusiwa kuingia kuutambua mwili ni yeye Njagu Aron, pamoja na nduguye pekee.
Familia ya marehemu ilifikia hatua ya kugoma kuondoka hospitalini hapo, ila nguvu ya kadri (reasonable force) ikaanza kutumika.
Familia ya marehemu ilifikia hatua ya kugoma kuondoka hospitalini hapo, ila nguvu ya kadri (reasonable force) ikaanza kutumika.
Swali: Ni kwanini manjagu walishiriki sana tukio hili tena wakiwa na silaha?
Siku pekee ambayo mdogo wa marehemu aliruhusiwa kuingia kumuona marehemu, alikuta vitu vya ajabu mwilini kwa marehemu, na ni siku hiyo ambayo mwili ulikua unasafirishwa kwenda kwa mazishi Moshi.
Siku pekee ambayo mdogo wa marehemu aliruhusiwa kuingia kumuona marehemu, alikuta vitu vya ajabu mwilini kwa marehemu, na ni siku hiyo ambayo mwili ulikua unasafirishwa kwenda kwa mazishi Moshi.
Ni kwa nini mwili wa marehemu ulikaa muda mrefu hospital ya manjagu? Bila ndugu wa marehemu kuruhusiwa kuuona.
Wakati haya yakiendelea, Njagu Aron. J alifanya utaratibu wa kununua shamba jipya huko Moshi, kwa gharama ya zaidi ya Mil. 20 wiki moja kabla.
Uamuzi wa mahali pa kuzikwa, ukatoka kuwa marehemu atazikwa katika shamba hilo lililo mbali kabisa na makazi ya watu wala historia
Uamuzi wa mahali pa kuzikwa, ukatoka kuwa marehemu atazikwa katika shamba hilo lililo mbali kabisa na makazi ya watu wala historia
Yaani kwa mfano, unaishi Dsm, wazazi wenu pande zote wapo Moshi, kisha ukamzike mkeo kwenye shamba jipya ulilonunua wiki moja kabla ya kifo chake, nje ya mji kabisa ambako hakuna makazi ya watu porini.
Hali ya kukuta sehemu za mwili wa marehemu zimeharibiwa na zingine kunyofolewa (sehemu za siri) ni hali ambayo iliwashtua sana familia ya marehemu, na kuanza kuzua taharuki nyingine kubwa sana.
Siku ya mazishi, bus la manjagu lilifika msibani na manjagu wa kutosha, wakiwa na silaha, waombolezaji wote wakiwa chini ya ulinzi haswa familia ya marehemu, (huko maporini).
Kwa hali ya shida, presha na mshtuko....mama mzazi nae akalala mauti sababu ya depression
Kwa hali ya shida, presha na mshtuko....mama mzazi nae akalala mauti sababu ya depression
Mama hakuweza kukubali hali ya kumkosa binti yake, hakuwahi kuwa sawa baada ya kifp cha bintiye, karibu mwaka mzima alisumbuliwa na mawazo na kutokubali hali, huku hakuna uchunguzi ukifanyika.
Nuru ikafifia, hatimae nae akaaga dunia mwishoni mwa mwaka 2023.
Nuru ikafifia, hatimae nae akaaga dunia mwishoni mwa mwaka 2023.
Hii familia ina haki ya kupewa nafasi ya uchunguzi wa kile wanachotilia mashaka.
Ikiwa haki itaamua hakukuwa na mashaka yoyote, basi iwe kheri, ikiwa kuna mashaka, basi haki ikatendeke na mahakama ziamue haki hiyo.
Ikiwa haki itaamua hakukuwa na mashaka yoyote, basi iwe kheri, ikiwa kuna mashaka, basi haki ikatendeke na mahakama ziamue haki hiyo.
Loading suggestions...