KUTAPELIWA DAR NI SUALA LA MUDA TU. ๐๐ฟ
Short story. #Thread.
Mwaka 2020 kipindi nasoma degree pale Udsm nilikua nafanya biashara ya kuuza simu used online hasa kwenye mda wangu wa ziada ili kujipatia hela ya ziada maana boom lilikua halitoshi.
Please RT.
Short story. #Thread.
Mwaka 2020 kipindi nasoma degree pale Udsm nilikua nafanya biashara ya kuuza simu used online hasa kwenye mda wangu wa ziada ili kujipatia hela ya ziada maana boom lilikua halitoshi.
Please RT.
Namshukuru Mungu kazi ile mimi binafsi ilinilipa sana na nilikua napata hela ya ziada. Kwani nilikua nanunua simu used kwa wanachuo waliofulia kisha nazipost mtandaoni iwe ni jiji.com au facebook market place. Basi mteja akiona kule anakupigia mnakutana unamuuzia
So nikinunua 150k nikauza 190k inakua ni faida 40k. So siku biashara ilikubali ilikua nauza mpaka simu 4 au 5 kwa siku za weekend au mbili kwa siku za kati kati ya wiki.
Biashara yangu ilikua tu fresh mpaka ikamvutia mwanangu mmoja anaitwa Ginimbi (Jina lake halisi nalificha)
Biashara yangu ilikua tu fresh mpaka ikamvutia mwanangu mmoja anaitwa Ginimbi (Jina lake halisi nalificha)
Aliponifuata nilimwelekeza safi akawa anauza pia. Yeye alikua anauza na laptop used pia so ikawa kadri siku zinavyozidi kwenda akawa anauza na kupata faida. Na yeye hakuwa na boom kabisa so ilimsaidia sana kujiboost kiuchumi.
Unapoendelea kusoma story hii
Nifollow @Deodravis
Unapoendelea kusoma story hii
Nifollow @Deodravis
Katika kufanya biashara hiyo mimi namshukuru Mungu sikuwahi kutana na janga la kutapeliwa ila jamaa yangu ikamtokea siku moja. Na kilichomponza ni ubinafsi. ๐๐
Siku hiyo tumekaa campus hatuelewi hili wa lile jamaa akawa anaongea sana simu za pembeni kumbe bhana kapata dili.
Siku hiyo tumekaa campus hatuelewi hili wa lile jamaa akawa anaongea sana simu za pembeni kumbe bhana kapata dili.
Alikua na mwanae anasoma IFM anamdai kama 20k so jamaa akawa anauza simu yake moja Sumsung A51 kwa 400k ko akawa amemgei jamaa picha aipost so jamaa akaipost kwa 550k na akapata mteja Ubungo maziwa. ๐๐ sasa faida yake 150k +20k anayodai 170k hivi so akanificha ili tusigawane ๐
Basi yule jamaa ake wakawa wamepanga kukutana Ubungo mwendokasi majira ya saa nane hivi mchana. Basi jamaa akawa anatafuta namna ya kunikwepa akapige hyo dili. Basi kama saa sita hivi alikuja pale tulipokaa mwanangu mmoja anaitwa Profesa (Jina lake halisi kapuni)
Akaleta tambo za draft na mimi kwenye draft sipendagi dharau. Tambo zilipozidi nikaona isiwe kesi tuweke battle tuingie kitaa tutafte draft tukakipige. Basi tukakubaliana twende Mawasiliano karibu na getho kwake kuna kijiwe. So Ginimbi yeye akapata upenyo wa kwenda kupiga dili
Basi tukaenda mpaka Kijiweni kukipiga alipofika pale akatuaga kama anaenda kumpokea jamaa. Sasa kwa sababu najua kuwa jamaa ni mtu wa hizo biashara nikamtania oyaa kama dili la simu rudi hata na 5k basi akasema fresh si anajiaminisha faida 150k tayari.
Basi akafika mwendokasi akampokea jamaa ake toka kigamboni. Tayari wanasogea Ubungo maziwa kukutana na mteja wao. Maake apo kwanza ncheke ๐. Yule mwanae alikua na Simu mbili hiyo A51 na Note 10 mpya kipindi hiko bei yake kama 900k hivi. Kumbuka biashara ni ile A51 ya 550k
Wakawasiliana na mteja wao wakakutana nae. Ni jamaa fulani hivi gentle amependeza af anasalimia kila mtu.๐ Picha linaanza akawaambia kuwa yeye hela ameacha nyumbani ko akaikagua simu af akawapeleka kwenye duka moja alilodai kuwa ndio sehemu yake ya kazi akaiweka chaji kutest.
Uchangamfu wake na kuongea na kila mtu kulifanya jamaa wasimtilie shaka na kuamini kuwa lile ni eneo lake la kazi. Ile A51 ilikua na chaji 21% yule mteja akashauri waiache pale dukani iendelee kuchajiwa af wao waongozane home kufuata hela. Ginimbi na mwanae wakakubali.
Wakiwa njiani kama kawaida yule jamaa (mteja wao) anasalimia ad boda boda. Basi katika kwenda jamaa ake ginimbi akawa anatumia ile Note 10 yake yule mteja wao alivyoiona akauliza hilo tambo gani wakamwambia Note jamaa akawa excited sana.
Akawaambia kuwa kuna sister ake anaipenda sana hiyo simu na ameitafuta dukani kama wiki lililopita amekosa. So akawauliza bei kama angeitaka wangemuuzia bei gani. Yule jamaa ake Ginimbi akasema yeye ile haiuzi. Ila akamwambia dukani inauzwa 950K. Basi jamaa akakubali kinyongeee.
Wakaenda wakafika mahali Yule jamaa aliposema ni nyumbani. Palikua na gate ila mlango wake mdogo uko wazi. Jamaa akawaambia wasubiri hapo jamaa wakasubiri jamaa akaingia ndani. Walisubiri kidogo jamaa akatoka nje. Cha kushangaza hakuwa na hela mkononi wala nini ๐
Akaja akawaambia kuwa dada yake yuko ndani na amemuambia kuhusu note 10 yao na yeye yuko tayari kutoa 1M ko wamuuzie nayo. Basi jamaa yake Ginimbi si akaingia tamaa akaona fresh kuuza kwa 1M maana alinunua 900 na amekaa nayo kama miezi mitatu kuuza 1M itampa faida 100k
Na ataenda kununua nyingine. Basi akasema mwambie alete hela. Yule jamaa akaingia ndani. Huku mwanangu ginimbi na mshikaji wake wanachekelea kusubiri faida. Lakini wakati wanaendelea kupeana excitement jamaa akarudi tena akasema kuwa sister ake anataka aione pia simu.
Jamaa hawakuuliza mara mbili akili yao ipo kwenye faida basi wakampa nayo jamaa akaenda nayo ndani wao wakabaki nje kusubiri hela ya simu zote mbili. Note 10 na ile waliyoiacha dukan kule A51. Walikaa dakika 5, 10, 15 30 jamaa hatoki ๐๐ wakataka kuingia ndani ya geti wakasita
Wakajipa moyo jamaa atatoka wakati wakiendelea kujiuliza mara kuna jamaa wawili wakawapita wakaingia kwenye lile geti wakaenda ndani. Hawajakaa sawa wakapita tena wengine watatu wakaingia, mara mmaza mwingine tena akaingia mmh wakajiuliza mbona watu wengi wanaingia pale aisee
Kuingia na wao kucheki wanagundua kuwa ile ni njia imepitiliza. Ingawa ni nyumba ya mtu ila watu hutumia kama chocho kupita kutokea upande wa pili. Na kumbuka hapo ilikua zishapita likanakiribia lisaa maskini. Jamaa wakapagawa. Wakajua washapigwa sasa nini wafanye.?
Wakagawana mmoja afuate njia na mwingine arudi mbio dukani waliko acha simu nyingine. Basi yule jamaa ake ginimbi akafuata chocho na ginimbi awahi shop. Sasa ukizingatia lile wenge la kutapeliwa plus mtaa ule ni mgeni kwake mwanangu ginimbi akapotea njia waliyokuja nayo ๐
Mpaka alipokuja kutoboa kule mwanae alikua ashafika pale shop na walikua washachelewa. Sasa wanakuuliza yule muuza duka (alikua mdada) anasema yule jamaa kashachukua simu kitambo na hamfahamu na wao pale huwa wanatoa huduma ya kuchaji simu. Na kweli wanabango linajieleza.
Kwahyo wakachoka, wakaenda kuwauliza boda nao wakasema nao walishangaa kuona jamaa anawapa gwara kama anawajua na wao ndio mara ya kwanza kumuona. Basi wakatafuta sehemu wakakaa yule jamaa wa kigamboni analia ๐ kaibiwa simu mbili A51 na Note 10 Hasara yake ni kama 1.4M
Basi walikaa pale kwa muda kisha wakaanza kusepa mdogo mdogo jamaa akapande mwendokasi arudi Kigamboni na mwanangu arudi zake getho Mwenge. Mi niko zangu ado ado narudi getho riverside nawaona wanatembea kuelekea mwendokasi kinyongeee oyaa usiombe ikukute.
Wanasema there is always a bad day in life. So tunapeana stories kama hizi ili siku ukikutana na hali kama hii ushtuke mapema.
MWISHO WA STORY.
Follow @Deodravis
MWISHO WA STORY.
Follow @Deodravis
Loading suggestions...