47 Tweets 61 reads Jul 15, 2023
Wakati mwingine Music huleta Amani, Burudani na Ujumbe mkubwa.
Mwaka 2015 nilikuwa napenda kusikiliza wimbo wa LUCKY DUBE uitwao "It's not easy"
Because I was tortured by love
Siku kadhaa mbele nilikuja kusikia mambo ya kuhuzunisha yaliyomuhusu msanii LUCKY DUBE
Ya kwamba👇
Siku ya tar 18/10/2007 ndani ya jiji la JOHANNESBURG, majambazi wa4 walikuwa wakiisaka gari aina ya chrysler 300c.
Lengo likiwa ni kuiba gari na kwenda kuiuza walipopajua wao.
Baada ya muda kupita, waliiona gari waliyokuwa wakiitafuta ikikatiza kwenye mitaa ya ROSETTENVILLE👇
Majambazi hao wakaifuata gari hiyo na kuimiminia risasi zilizopelekea kukatisha uhai wa mtu aliyekuwa ndani ya gari hiyo
Mtu huyo ni LUCKY DUBE
Na baada ya kufanya hicho walicho kifanya hawakuiba gari hiyo, bali jambo kubwa waliloliona ni kutokomea kusiko julikana👇
A strange thing after one hour
Majambazi hawa wakarejea tena eneo la tukio ili kujihakikishia Je Hakukuwa na mtu aliyewaona.
Kisha baada ya kujihakikishia hakuna mtu aliyewaona, wakaamua kwenda night club huko wakanywa na kugonga cheers bila hofu.
It seems normal to them👇
Kwa kuwa Story hii niliwahi kuisoma miaka hiyo ndani ya website ya "IOL"
Ilinifanya nibaki na maswali mengi yenye utata.
lakini swali kubwa ni why majambazi hao hawakuiba gari ya DUBE kama ilivyo sehemu ya mpango wao.?
Na why walirudi tena eneo la tukio.?
Niliwaza.
Perhaps👇
there was something else that brought them back to the scene.
Udadisi na maswali yenye utata yalitawala kichwa changu.
Leo hii nimeona si mbaya kama tukisonga pamoja na LUCKY DUBE.
Katika kuzaliwa kwake, hustle zake, umaarufu wake mpaka kifo chake chenye utata mkubwa👇
Mwaka 1964 ni mwaka ambao LUCKY DUBE aliingia katika vilindi vya dunia hii.
Kwa majina ya Document anaitwa LUCKY PHILIP DUBE, Amezaliwa 03/08/1964 huko MPUMALANGA nchini SOUTH AFRICA.
LUCKY DUBE ni mtoto aliyesadikika atakufa ndani ya muda mfupi tu baada ya kuzaliwa👇
Ilikuwa ni baada ya mama wa LUCKY DUBE kupata watoto kadhaa ambao wote walifariki punde tu walipo zaliwa.
Ilipofika zamu ya kujifungua LUCKY DUBE mama huyu hakumpa jina mtoto wake badala yake alimuachia Mungu na kusema..
"ikiwa utamkuza nitampa jina linalo kupendeza"
Mwaka👇
Mmoja ukakatika mtoto bado anaishi, mama huyu aliona ajabu maana watoto wote walikufa siku kadhaa baada ya kuzaliwa.
Mama huyu akiwa ameshakimbiwa na baba wa mtoto. ndipo alipoamua kumpatia mtoto huyu jina la kizulu la "Inhlanhla" likiwa na maana ya Bahati.👇
Inhlanhla alipoanza kujitambua, aliomba kazi ya kutunza bustani kwa wazungu.
Kazi akapata ila aliulizwa maana ya jina lake, akasema bahati mabosi zake wakamuita Lucky.
Mara zote Dube alisikia akiitwa Lucky na mabosi zake, from there ikawa anajitambulisha kwa jina la Lucky.👇
Hata shule alibadilisha jina kutoka Inhlanhla na kuja Lucky.
Japo maisha yakwao hayakuwa rafiki LUCKY DUBE alijitahidi kujisukuma kwenda Shule mwenyewe, sababu aliachwa na bibi yake huku mama👇
Yake akiwa amekwenda kutafuta vibarua ndani ya jiji la DURBAN.
Dube akiwa na bibi yake, alipambana mara zote ili kuhakikisha analeta kitu nyumbani.
Alikuwa na tabia akitoka shule anapitia kwa bosi wake, ambao ndio hao mnawaita makaburu.
Siku hiyo alivyo fika kwa bosi👇
alishangaa anaitwa sebuleni, ni ajabu miaka hiyo mtu mweusi ulikuwa huwezi kukaa sehemu moja na wazungu.
Zaidi ni hapo South Africa sababu bado walikuwa wametawaliwa na makaburu.
Alipofika sebuleni akaambiwa atoke, DUBE akatoka.
Kisha zikapita kama dakika10 👇
Dube aliitwa tena aende sebuleni alipofika alionyeshwa waya mbili za umeme ambazo zilikuwa zimekatwa.
Akaambiwa aishike moja na nyingine kisha akaambiwa azigusanishe, Dube alifanya ivyo.
Kilichotokea Dube alirushwa na umeme mkali uliokuwa kwenye waya hizo, alidondoka chini👇
kwa kishindo.
Alitweta akiitafuta pumzi huku akiwasikia kwa mbali makaburu wakimcheka na kuwaambia watoto wao.
"This is how it works"
Kwamba LUCKY DUBE alitumika kama mfano kwa watoto wa makaburu kujifunza jinsi umeme unavyo fanya kazi.👇
Tokea hapo Dube aliwaona makaburu na wazungu wote duniani kama maadui, watu wabaya na wenye roho mbaya.
Miaka ikakatika na baadae alipata nafasi ya kujiunga kwenye kundi la Sky Way Band.
Hapa alianza kuzungumzia maisha kupitia muziki, Dube 👇
Akiwa ndani ya kundi hili alianza kuimba kwa kutumia Lugha ya kizulu.
Maisha yakawa ndio hayo, kanisani aliimba muziki, mtaani aliimba muziki..
Akatoa wimbo uitwao "Zulu Soul." Na baadae kama kundi wakaachia album yenye jina la "Baxoleleni, huku mwimbaji mkubwa akiwa ni DUBE👇
Hizi ni nyakati ngumu kwa LUCKY DUBE kwani japo alijiunga katika kundi hilo lakini maisha bado yalimpiga.
Alijihudumia kila kitu mwenyewe na niwakati huu pia ndio wakati ambao alipaswa kumsaidia mama yake na bibi yake nyumbani..
Mama alirudi nyumbani baada ya👇
Kusumbuliwa na kifua ivyo hakuweza tena kufanya vibarua, Kwa kifupi familia ikawa inamtazama LUCKY DUBE kama mboni.
Who knows your problems.?
No one knows..
Licha ya matatizo mengi ya kifamilia kumzonga Dube hakuacha kujifunza muziki kila kukicha
Ilipofika👇
Mwaka 1984 Dube alionekana kwenye movie ya GETTING LUCKY.
Mwaka uliofuata 1985 akatoa album ya "Rastas Never Die"
Hii ikawa chukizo kwa makaburu, album ikafungiwa.
1986 akatoa tena album ya "Think About the Children" or "Born to suffer" Hii ikaenda
Hapa taa👇
ya Dube ilianza kuwaka.
Na nyakati hizi ndizo alizohamia kwenye mji wa Johannesburg rasmi.
Akawa anatoa nyimbo za ukombozi, kutetea haki za watu.
Kuna siku askari wa kikaburu walimvamia na kumpiga virungu bila sababu.👇
Dube aligundua source ya kipigo hicho ni nini,, alijua wazi ni nyimbo zake zinazoikosoa serikali ndio chazo cha kipigo hicho.
Dube hakuacha kuimba kwa lugha laini inayoburudisha, kukosoa na kufundisha.
Akatoa nyimbo yake aliyoimba kwa kizulu USIZI.
Ilipendwa na ikaenda..👇
LUCKY DUBE taa yake ikazidi kumulika na mara hii hakutaka kabisa kutumia lugha ya kizulu katika nyimbo zake.
Na badala yake akatumia Lugha ya kiingereza moja kwa moja ili nyimbo zake zisikilizwe duniani kote na si South Africa pekee.
Ni kama alivyo taka....👇
Mwaka 1987 akatoa album ya SLAVE yenye nyimbo kama..
~Slave
~Back to My Roots
~Oh My Son (I'm Sorry)
~Rastaman
~Let Jah Be Praised (Igzebier)
~The Hand That Giveth
~I've Got You Babe
Hii album alimpeleka Lucky Dube duniani, akasikilizwa na kila lika👇
akawa maarufu ndani ya South Africa na njee ya South Africa.
Dube akabamba, akajitafuta na akajipata, uimbaji wake uliogusa maisha halisi ya watu, ulifanya asikilizwe na watu wengi kutoka pande zote.
Historia Alianza kuiandika kwa kujaza watu wengi zaidi kwenye show zake👇
Sasa akawa anasikika zaidi katika ulimwengu wa muziki wa Reggae huku wasanii kama Peter Tosh, Bob Marley na Jimmy Cliff wakianza kupotea katika mazungumzo ya watu.
Kijana huyu kutoka South Africa sasa akatazamika pengine ndiye mrithi wa Bob Marley👇
Dube alijitengenezea utofauti fulani katika uimbaji wake..
Ni zile sauti za wanawake waliosikika mara kwa mara wakiimba Choruses kwenye nyimbo za DUBE ni wanawake watatu ambao uongozi wa Dube uliwaita...
"Mothers of Soweto which never sleeps"
Yaani wamama wa Soweto ambao👇
hawalali kamwe.
Ni sababu wanawake hao walipohitajika studio saa na muda wowote walifika bila kukosa
Pia Dube alipokwenda kufanya show iwe nje au ndani ya nchi ni wao ndio walipangilia style za uchezaji huku wakiimba kama backing vocalist.
Dube aliwaita the voices of revival👇
Akimaanisha sauti za uamsho.
Kupitia "OKTV Awards" LUCKY DUBE alishinda tunzo nne kupitia album yake ya PRISONER.
Yenye nyimbo Kama...
~Prisoner
~Dracula
~False Prophets
~War And Crime
~Remember Me
~Don't Cry
~Jah Live
~Reggae Strong
DUBE hakuishia hapo.👇
Mwaka 1991, alitembea nchi tofauti.
Kupitia nyimbo zake alichukuliwa Kama mtu anayetangaza amani, upendo na kuoneana huruma Utu.
Alikwenda Japan na Australia, alikuwa akihitajika kama source ya kuwaliwaza watu au ufunguzi juu ya taasisi ama tamasha la kitaifa.👇
DUBE akaendelea kusonga mbele kwa bidii zaidi, hakika aliushangaza ulimwengu.
Mwaka 1992, Dube alikuwa Mwafrika Kusini wa kwanza kufanya show kwenye tamasha la Sunsplash nchini Jamaica.
Wapo wa Jamaica waliosema Dube ana asili ya Jamaica huku wa Zimbabwe nao👇
Wakisema Dube ni wa kwao, kwa kudai ya kwamba wazazi wa Dube wana asili ya Zimbabwe.
Mwaka 1993 Dube akaja na nyimbo iliyoitwa Remember me.
Akijaribu kujizungumzia yeye alivyoachwa na baba yake lakini pia hata watu wengine waliopitia malezi ya kukosa baba.👇
Dube aliendelea kuachia nyimbo kila kukicha, ila mwishoni mwa 1993 matukio ya uhalifu yalikuwa mengi sana South Africa.
Watu walikuwa wakidai uhuru dhidi ya mkaburu aliyekuwa hataki kubanduka ndani ya nchi hiyo.
Ila katika kudai uhuru huo watu walipiga pesa na zaidi👇
Ni watu weusi wenyewe kwa wenyewe waliibiana na kupelekea wengine mpaka kupoteza uhai wao.
Raia walimiliki silaha kiholela holela, jambo lililofanya mauaji kutokea kila kukicha.
Uhalifu, madawa ya kulevya na wizi wa silaha ulitawala South Africa.
Aggravated crime.👇
Tar 27-04-1994 nchi ya South Africa ilipata uhuru wake kutoka kwa mkaburu aliyeitawala nchi hiyo kwa miaka mingi.
Ila baada ya uhuru kupatikana, matukio ya uhalifu bado yaliendelea hayakukoma..
Ndipo March 31-1995 LUCKY DUBE akajana na👇
album yake ya TRINITY yenye nyimbo Kama..
~Trinity
~Feel Irie
~Puppet Master
~You Got No Right
~Affirmative Action
~Big Boys Don't Cry
~Rasta Man's Prayer
~God Bless the Women
~My Brother, My Enemy
Sasa hii nyimbo ya My Brother, My Enemy👇
Anazungumzia maisha yake yote jinsi alivyo muona mzungu ni adui yake.
Lakini baada ya kuona matukio ya mauaji kila kukicha, tena weusi kwa weusi yaani wao kwa wao.
hapo akagundua..
Kwamba hakujua hata mtu mweusi aliyehisi ni ndugu yake kumbe anaweza kumuua, au👇
Kumfanyia uhalifu.
Not every black man is my brother
Not every white man is my enemy
Dube anaandika tena katika wimbo uliobeba jina la album hiyo Trinity
Katika nyimbo ya Trinity Dube anaandika kwa kumuunga mkono Mandela juu ya kumsamehe mkaburu..
kwamba👇
Mkaburu baada ya kusamehewa, asilale na bunduki yake mkononi, akidhani perhaps waafrika kusini wanaweza kumvizia na kumuua.
Awe na amani
Mwafrika kusini atamfuata mkaburu ili kujifunza kuhusu watu weupe na mkaburu atamfuata mwafrika kusini kujifunza kuhusu watu weusi.
Dube👇
anasisitiza we'll unite" tutaungana" kwamba licha ya yoote yaliyotokea bado wanapaswa kuwa kitu kimoja.
Maisha yakasonga lakini matukio ya uhalifu bado hayakukoma nchini South Africa.👇
LUCKY DUBE aliendelea kukonga nyoyo za watu na kutikisa anga la muziki.
He has a musical soul.
No doubt hata mimi mwandishi ninakiri kwamba Dube alikuwa na nyota yenye uwezo wa ajabu na nuru yenye mwanga wa namna yake.
Kuna mzee👇
Mmoja aliwahi kuniambia, Lucky Dube ni dirasa, ni somo na pia ni shule kubwa watu wanapaswa kujifunza kupitia nyimbo zake.
Sikuwahi kumuelewa Mzee yule ila sasa ninayakumbuka maneno yake na ninayaelewa maneno yake...
Miaka ikasonga.. na ilipofila mwaka 2000👇
Nchi ya South Africa kwa mara ya kwanza ikapata kamishna mweusi wa Kitaifa wa Huduma ya Polisi ya Afrika Kusini.
"First National Commissioner of the South African Police Service"
Huyu ni Mzee JACOB JACKIE SELEBI maarufu kama JACKIE SELEBI.
Bwana JACKIE SELEBI baada ya👇
kushika wadhifa huo akaanza kufanya kazi yake huku akiwa chini ya Rais THABO MBEKI aliyerithi kiti cha NELSON MANDELA mwaka 1999.
Lakini siku baada ya siku matukio ya uhalifu yalizidi kuendelea bila kukoma.
Miaka ikakatika na ilipofika mwaka 2007 yaani👇
Siku ya tar 18/10/2007 maisha ya LUCKY DUBE yakakatizwa kwa namna ya ajabu sana..
Yaani ghafla majambazi yakatokea na kummiminia risasi, kisha majambazi yakaondoka na baadae yakarudi tena eneo la tukio eti kuhakikisha kama hayakuonekana.
Perhaps hili ndilo kosa kubwa👇
Walilolifanya majambazi hawa....
Baada ya tukio kutokea taarifa zikawafikia askari kadhaa wa JOHANNESBURG ambao walikuwa ndani ya mtaa wa ROSETTENVILLE wakifanya doria.
Askari hawa wa kikosi cha doria ambao miongoni mwao kulikuwa na shushushu wa Kapteni MLOKO KGOMO👇
Everything you read in this story highlights the truth of LUCKY DUBE's life, his hustles, his fame to the truth of his death.
Stay safe kwa ground mambo ni mengi sana🙏
Usiache kunifollow as @wisdomjaykwa #wisdomjaykwa
End of the first Ep, Ep 02 itaendelea....

Loading suggestions...