Digital Nomad ( YT @mafolebaraka)
Digital Nomad ( YT @mafolebaraka)

@mafolebaraka

8 Tweets 11 reads Jun 21, 2023
Mimi ni mtumiaji mkubwa sana wa tools, Natumia tools kwenye masuala yangu binafsi na yahusuyo kazi .
Leo ngoja nikuandikie tools ninazozitumia zaidi kwenye simu yangu, Btw nyingi najua utakuwa huzifahamu
Dondoka nayo .....
1. Life Planner @LifePlanner_co
Kabla ya kuwajua hawa majamaa, maisha yangu yalikuwa shaghalabaghala. Kama ilivyo kwa freelancers wengine matumizi sahihi ya fedha, kuseti mipango na mkakati wa kuacha tabia hatarishi ni masuala ambayo yanatutesa kila siku.
....
Life planner nawatumia sana kupanga mahesabu yangu ya mwezi mzima, pia washkaji wamekua msaada sana kwangu kuondokana na tabia za kutomaliza kozi za mtandaoni na kuacha tabia ya kutokufanya mazoezi.
Version yao ya kulipia ndo nzuri zaidi
2.Pomofocus @pomofocus
Kuna katabia ka kushindwa kumaliza kazi kutokana na distraction mbalimbali kama mitandao ya kijamii na mazungumzo madogo madogo kalikuwa kananitesa.
Pomofocus wananisaidia kuweka timer kila ninapokuwa nafanya kazi yangu,Hii imenisaidia sana
3.Notion @NotionHQ
"Mjini mipango " Moja ya verse imetumiwa sana na wasanii wetu wa bongo fleva. Binafsi nina mipango yangu ya siri na wazi.
Doc na taarifa zangu muhimu zote huwa ninazihifadhi notion.Uzuri wa notion pia ni rahisi kushare na mtu documents zako.
4.Discord @discord
Mazungumzo yangu mengi hususani na wateja wangu wa AI na Crypto huwa nafanyia Discord.
Also mimi ni community manager by professionally na kama hufahamu Discord ni mtandao ambao primarly umetengenezwa kwa lengo la kutengeneza jumuiya.
5.Trello @trello
Moja ya tool bora ya project management duniani ni Trello, Vikolokolo vyangu vingi huwa naviendesha kupitia Trello.
Kwa leo niishie hapa

Loading suggestions...