46 Tweets 12 reads Jun 16, 2023
Siku ya Ijumaa tar 06-03-2020 Niliona Taarifa mitandaoni zikisema.
"RONALDINHO akamatwa nchini PARAGUAY kwa kutumia pasipoti bandia"
Kudadisi kukazuka na haraka nikawaza..
Kwanini RONALDINHO atumie pasipoti bandia.? na alienda kufanya nini huko PARAGUAYπŸ‘‡
Nikapita kwenye websites tofauti na ndipo nilipokuja kupata taarifa za awali zilizosema..
RONALDINHO na kaka yake aliyefahamika kwa jina la ROBERTO MOREIRA ya kwamba walinyang'anywa passport zao za kibrazil na serikali ya Brazil.
Hapa nikawaza tena inawezekanaπŸ‘‡
Kunyang'anywa kwa pasipoti zao halali ndio sababu ya RONALDINHO na Ndugu yake kutumia pasipoti bandia ili kuingia Nchini PARAGUAY
Pia udadisi wangu ulitaka kufahamu je! Kulikuwa na ishu gani ya muhimu huko PARAGUAY mpaka RONALDINHO na ndugu yake wafanye icho walicho kifanyaπŸ‘‡
Na zaidi nikajiuliza
Serikali ya Brazil ilifanyiwa uharifu gani na RONALDINHO mpaka kumnyang'anya passport na nduguye ROBERTO MOREIRA.
Ni maarufu na aliipeperusha vyema bendera ya nchi yake, why ifikie hatua anyang'anywe passport.
What crimes did he commit?
Ndipo nilipoπŸ‘‡
Pata kiu ya kufahamu mapito ya RONALDINHO.
Kwa majina ya Document anaitwa RONALDO DE ASSIS MOREIRA, amezaliwa PORTO ALAGRE huko BRAZIL,
Ni wa mwisho kwenye familia ya watoto wa3 Kaka yake anaitwa ROBERTO DE ASSIS MOREIRAπŸ‘‡
na dada yake ni DEISI DE ASSIS MOREIRA mama Dona Miguelina baba yake ni JoΓ£o de Assis Moreira
Baba wa RONALDINHO alikuwa akifanya kazi kwenye shilika la meli, lakini pia alikuwa anacheza mpira kwenye club ya Esporte Clube Cruzeiro ambayo kwa sasa ni Cruzeiro Esporte Clube.πŸ‘‡
RONALDINHO akiwa na umri mdogo alipenda kuongozana na kaka yake kwenda uwanjani kucheza mpira.
Siku moja kwa bahati mbaya alianguka na kuumia, alilia kwa maumivi kaka akamwambia anyamaze.
"Football is a game that brings happiness"
RONALDINHO akanyamaza na safari ya kurudiπŸ‘‡
nyumbani ikaanza, wakiwa njiani ghafla kijana mmoja anawakimbilia na kumuita kaka wa RONALDINHO.
"Roberto!! Roberto!! Baba yako amedondoka"
Nitaarifa zisizo nzuri kwa ROBERTO na mdogo wake RONALDINHO, hii ni siku waliyompoteza baba yao, Ni baada ya baba kupatwa naπŸ‘‡
Mshituko wa moyo akiwa kazini na alipowahishwa hospital na wafanyakazi wenzie akawa amesha fariki tayari.
Huu ndio mwanzo wa ROBERTO kuyabeba majuku ya familia, baba ameenda yeye ndiye mkubwa ivyo alipambana kwa kila namna kuhakikisha wadogo zake na mama yake wanakuwa salama..πŸ‘‡
ROBERTO aliweka juhudi zake kwenye mpira na kama ilivyo kawaida juhudi zako haziwezi kukuangusha,,
Akapata bahati ya kusajiliwa kwenye club ya GREMIO na hapo ndipo milango yake kwenye ulimwengu wa soka ikafunguka.
Akawa mchezaji mahili uwanjani akatumia jina laπŸ‘‡
babu yake ASSIS, alitumia jina hilo kama heshima katika familia yao.
Angalau sasa aliweza kuyamudu majukumu ya familia, waliishi nyumba nzuri na wadogo zake walikwenda shule kupitia yeye.
Siku zilisonga lakini siku moja akiwa kwenye mchezo alipata Jeraha la mguuπŸ‘‡
Alihisi ni tatizo dogo ila kadri muda ulivyokwenda maumivu makali yakazidi na walipokwenda hospital akaambiwa hawezi tena kucheza mpira Otherwise ataupoteza kabisa mguu wake.
Milango iliyofunguka ikafunga.
ROBERTO akiwa kama kaka tegemezi alivurugwa na akawaza nini afanyeπŸ‘‡
ili familia isidhalilike.
Akamtazama mdogo wake kwa jicho la3, shilingi moja imezama, akajipa moyo perhaps anaweza kuitumia shilingi ya mwisho aliyobaki nayo mkononi mwake.
ROBERTO akajiapiza mwenyewe kwamba mdogo wake ni lazima ajue mpira.πŸ‘‡
ROBERTO akamuita mdogo wake RONALDINHO na akamtaka atumie jina hilo ili kujitofautisha na jina lake la asili RONALDO, kulikuwa na kina RONALDO wengi miaka hiyo ivyo motive ya ROBERTO ni kwamba alitaka jina la mdogo wake liwe tofauti na wengine.
RONALDINHO hakujua kamaπŸ‘‡
Kaka yake anamtazama kama shilingi iliyobakia, mazoezi ikawa ni sehemu ya maisha yao.
ROBERTO alitega RONALDINHO aliporudi Shule tu! Ni kubadilisha nguo na kwenda kiwanjani kufanya mazoezi.
Kutokana na Umri wa RONALDINHO alihisi pengine huo ni mtindo wa maishaπŸ‘‡
Ya watu wote duniani.
Akajikuta anapenda mpira na alifurahia mara zote kuucheza mpira
Miaka ikasogea, RONALDINHO Akafanyiwa mpango na kaka yake na kujiunga na Club ya GREMIO.
Club ambayo alikuwa akicheza kaka yake kabla ya kupata shida ya mguu.
Huu ndio ulikuwa mwanzoπŸ‘‡
wa taa ya RONALDINHO kuwaka.
Ilikuwa ni mwaka 1998 Brazil ikazungumza kuhusu RONALDINHO, GREMIO ikawa ni club inayopendwa siku baada ya siku nchini Brazil.
Club ya GREMIO Ikazidi kujizolea mashabiki walio vutiwa zaidi na uchezaji wa RONALDINHOπŸ‘‡
Na hapo ndipo
mashabiki wa timu ya GREMIO wakamuongezea jina lingine la GAUCHO, jina lililotokana na asili ya mtu mmoja mchunga ng'ombe aliyewahi kutembea umbali na umbali, jasiri na mwenye mafanikio makubwa huko America ya kusini.
Ilipofika mwaka 2001 RONALDINHOπŸ‘‡
alijiunga na club ya Paris Saint-Germain "PSG" hapa aliwashangaza watu kwa style zake za uchezaji jambo lililofanya Club ya Barcelona imtazame kwa jicho la3.πŸ‘‡
Hakikupita kipindi mwaka 2003 RONALDINHO akajiunga na club ya Barcelona taa ya mafanikio ilizidi kuwakaπŸ‘‡
na kumulika pande zote za dunia.
Ukawa ni wakati mzuri kwa RONALDINHO Alianza kupata mafanikio makubwa kupitia mpira.
Kaka yake ROBERTO akiwa kama wakala wake alihakikisha mara zote anakuwa karibu na RONALDINHO ili ikiwa kuna changamoto anapitia aweze kufahamu.πŸ‘‡
RONALDINHO alishinda taji la Laliga mwaka 2004-2005 kisha akashinda kombe la mabingwa la UEFA.
2005 hiyihiyo akapata mtoto wa kiume na mchumba wake Janaína Mendes na mtoto wao wakampa jina la JOÃO
RONALDINHO akawa wamoto kwenye ulimwengu wa soka, akapendwaπŸ‘‡
na wachezaji na kila mtu alitamani kuwa karibu naye, Rafiki yake mkubwa alikuwa ni SAMUEL ETO'O
RONALDINHO Wakati wote huo alikuwa akivutiwa na kijana mmoja aliyemuona akifanya mazoezi kwenye matawi ya Barcelona C na B na mwisho RONALDINHO akalazimisha kijana huyo aungweπŸ‘‡
kwenye Club ya Barcelona FC.
Huyu ni Lionel Messi
Mwaka 2007πŸ‘‡
RONALDINHO Alianza kupata majeraha ya mara kwa mara jambo lililofanya asiwe vyema katika michezo yake.
Mara zote hizo alimsisitiza Lionel Messi kucheza kwa juhudi na auchukulie mchezo kama ni sehemu ya Furaha, ya kwamba asiogope wala asiwe na hofu.
Ilipofika 2008πŸ‘‡
RONALDINHO akatoka Barcelona na kujiunga na club ya AC Milan, 2008-2011 na club ya CR Flamengo 2011-2012.
Mwaka huo huyo 2012 alifunga ndoa na mchumba wake JANAÍNA ambaye tayari alipata naye mtoto.
Kisha akachezea tena kwenye Club ya AtlΓ©tico Mineiro 2012-2014πŸ‘‡
Taa ya RONALDINHO iliyowaka na kumulika duniani kote ilianza kuwa hafifu
Akacheza kwenye Club ya QuerΓ©taro na club ya Fluminense
Mwaka 2015 alirudi rasmi Brazil na kuendeleza maisha yake ya kisoka hapo, sijui kilitokea kitu gani ila yeye na mkewake JANAÍNA wakaachana
Na maraπŸ‘‡
Tetesi zikavuma yakwamba RONALDINHO anampango wa kuwa kiongozi katika jimbo fulani hapo Brazil.
Uwekezaji wake ulikuwa ni mkubwa katika nchi hiyo, haina ubishi pengine angekuwa mgombea angepita bila kupigwa.
Lakini ghafla wakaja wanawake wawili kwenye maisha yakeπŸ‘‡
Ambao ni Priscilla Coelho na beatriz souza hapa RONALDINHO akachanganya mafile akaanza kwenda puta, kila kukicha akawa ni mtu wa scandal na kuonekana kwenye kumbi za starehe na wanawake hao, wakati mwingine na wanawake wengine tofauti.
Ilipofika 2018 taarifaπŸ‘‡
Zikavuma ya kwamba RONALDINHO anataka kuwaoa wanawake hao wote kwa mpigo,
Uvumi ulipozagaa wanawake hao wakakili mbele ya waandiahi wa habari wapo tayari kuolewa kwa pamoja. Hii ikawa ni kashifa na kitu kilichofanya watu wazidi kumshusha hadhi RONALDINHO.
Lakini haikuwaπŸ‘‡
Kama ilivyozungumzwa RONALDINHO hakuwaoa wanawake hao, akaanza kuwapunguza taratiibu na ndipo wanawake hao walipoanza kwenda mahakamani wakitaka kugawana mali za RONALDINHO.
Fear woman...
Lakini pia sehemu za uwekezaji wake zilianza kuingia kwenye migogoro na kuitwaπŸ‘‡
Muwekezaji wa hovyo.
Sehemu nyingi alizowekeza zikagundulika ni hifadhi za wanyama na maeneo ya serikali, RONALDINHO akatolewa akili kwa kuitwa mla unga na mpenda wanawake.
Nchi yake mwenyewe ikaanza kumkaanga, kila mtaa wa Brazil ulikuwa ukizungumza mabaya ya RONALDINHOπŸ‘‡
Priscilla na beatriz wanataka mali mahakamani huku Serikali inazidi kumuandama kwa kuchukua maeneo yake ya uwekezaji, walimwengu nao hawakuacha kumsakama kwakifupi huu ulikuwa ni wakati mgumu kwa RONALDINHO na familia yake.
Hali ilikuwa tete zaidi baada yaπŸ‘‡
Siku moja kupigiwa simu Sehemu ya uwekezaji wake nyingine imezuiliwa, baada ya serikali kubaini wamekata msitu wa asiri na kumiliki sehemu hiyo bila leseni.
Walipofika la tukio yeye na kaka yake ROBERTO wakashindwa kuelewana na maafisa wa serikali wakaleta mzozo mwishoπŸ‘‡
wakanyan'nywa passport zao na kupewa kesi ya kuwapiga maafisa wa serikali "beating government officials"
Mzigo ukaongezeka kesi ya madai ya mali na kesi ya kuwapiga maafisa wa serikali na bado maeneo yake yakazuiliwa na zaidi hawawezi kutoka nje ya nchi
Mwishoni mwa 2019πŸ‘‡
RONALDINHO na Ndugu yake ROBERTO wakapata mwaliko kutoka kwa mfanya biashara maarufu Nchini PARAGUAY, huyu ni mwana mama Dalia Lopez.
Lakini pia kulikuwa na kitabu cha RONALDINHO walipaswa kwenda kukizindua Nchini Paraguay.
Ndipo unafanyika mpango waπŸ‘‡
Kuandaa passport, Dalia anaandaa passport mbili za kiParaguay zenye majina ya ROBERTO na Mdogo wake ambaye ni RONALDINHO zikisomeka kwa majina ya RONALDO DE ASSIS MOREIRA na ROBETRO DE ASSIS MOREIRA.
baada ya hati hizi za kusafiria kuwa tayari zikatumwa nchini Brazil na ndipoπŸ‘‡
RONALDINHO na kaka yake ROBERTO wanafunga safari na kuingia kwenye nchi ya PARAGUAY na kukutana na mfanya biashara Dalia Lopez.
Dalia alikuwa akifungua kampuni yake mpya ivyo mualiko wa RONALDINHO kuja katika nchi hiyo ilikuwa ni kupush au kuitangaza kampuni hiyo kimataifa.πŸ‘‡
Lakini pia RONALDINHO alipewa fulsa ya kutangaza kitabu chake kipya katika nchi hiyo ya PARAGUAY.
Baada ya kumaliza majambo yao yote, RONALDINHO na Ndugu yake wakawa tayari kwa kujiandaa ili kurudi Brazil na ndipo wanasikia mrango unagongwa mara maafisa kadhaa wakaingiaπŸ‘‡
Maafisa hawa wakajitambulisha ni watu wa Immigration "Uhamiaji" na kuwaomba passport zao ili kuhakiki majambo fulani.
Maafisa hao wakaziingiza namba za passport kwenye data zao na kugundua zinazoma majina tofauti na zaidi ni majina ya wafungwa wawiliπŸ‘‡
Walio swekwa gerezani miaka kadhaa nyuma.
Lakini pia passport hizo zilionyesha wao ni raia wa Paraguay, hili likawafikirisha maafisa..
Hata mimi linanifikirisha pia..
"Tokea lini RONALDINHO amekuwa ni raia wa Paraguay"
Hakukuwa na maelezo tena pingu ziliwahusu..πŸ‘‡
Hii ilikuwa ni Ijumaa ya tar 06-03-2020 taarifa zikasambaa haraka mitandaoni kwamba..
"RONALDINHO akamatwa nchini PARAGUAY kwa kutumia pasipoti bandia"
Mengi yakazungumzwa lakini taarifa hizi zilipowafikia Lionel Messi na Samuel Eto'o zikawaumiza vichwa.πŸ‘‡
Kesi ilipigwa danadana huku RONALDINHO na kaka yake wakiwekwa jela, wakiwa rupango waliishi kama wako njee kwani walikuwa na kila kitu.
Walikaa ndani kwa mwezi mmoja na kutoka njee kwa dhamana kwa msaada wa Lionel Messi na Samuel Eto'oπŸ‘‡
Huku baadhi ya maaskari wa Paraguay wakiomba picha kutoka kwa RONALDINHO, lakini bado alitakiwa kutumikia kifungo chake cha njee ivyo alikaa hotel kwa takribani miezi mitano, baada ya hapo akaruhusiwa kurudi Nchini Brazil.
Ilipofika February 20 2021πŸ‘‡
RONALDINHO akampoteza mama yake Mzazi, sasa amebaki na kaka, dada na mtoto wake wa kiume pekee.
Hajatangaza kuwa kwenye mahusiano na mwanamke yeyote tokea alivyoachana na wale wanawake wawili,
Kwa sasa anashirikiana vyema na Mzazi mwenzake juu ya kumuandaa mtoto waoπŸ‘‡
Wa kiume anayetamani siku moja awe kama baba yake.
Perhaps siku moja atakuwa mchezaji mkubwaπŸ’ͺ Yapo mengi ila haya ni machache kutoka kwa RONALDINHO GAOCHO
Stay safe kwa ground mambo ni mengi sanaπŸ™
Usiache kunifollow as @wisdomjaykwa #wisdomjaykwa

Loading suggestions...