10 Tweets 49 reads May 11, 2023
Vijana ambao mmehitimu vyuo nataka niwape taarifa. Inawezekana wengi hawawaambii ukweli.
Ajira Iko based on SKILLS na sio PROFESSIONS.
Jinoe zaidi kupata skills bila kujali level ya elimu ulonayo.
Na unapoenda kuomba kazi, kaombe kuonesha UWEZO sio elimu.
Wekeza kwenye UJUZI
Mimi nimesomea maswala ya Engineering lakini kwa asilimia zaidi ya 80 ninafanya kitu ambacho sio profession yangu.
Iko hivi:- Niliposoma chuo, Kuna kozi ambazo nilisoma mwaka 1,2 na 3 ambapo ndio zinanipa kipato.
Nilisoma Graphics, kupitia Photoshop CS3 wakati huo.
Nikajikuta naipenda sana. Nilikomaa nayo sana, na kujiongeza kwenye program zingine kama Ai, Pr, Id.
Lakini pia nilikomaa na Web design. Leo ni kitu kinachonipa income.
Lakini niliondoka na issue za Networking. Na hii kozi ilinifanya nijilipie ada mwaka wa mwisho na kumwambia
Mzee wangu apumzike afanye shughuli za maendeleo na kuwasomesha wengine.
Maana Mwalimu wangu alipenda kwenda nami kwenye fields zake. Na huko nikakomaa na kazi.
Leo hii issue za Routing Configurations, Cabling, Topologies sketching n.k ni vitu ambavyo navifanya sana.
Kiufupi ni kwamba Leo ninao uwezo wa kuishi kwa kutegemea
TALENTS, PROFESSION & SKILLS
Kilichonivusha katika nyakati ngumu sana ni SKILLS, na Sasa ndio imenifanya nijiajiri. Na maisha yanaendelea.
Uzuri wa skills haina bei elekezi. Bali unalipwa kulingana na VALUE uliyojipa.
Kuwa na skills fulani sio lazima uwe umesomea. Mfano, ofisini kwangu Nina msaidi ambaye anafanya issue za Graphics & Motion graphics Design lakini professionally ni DAKTARI (CO)
A guy is very pushing things great.
So, unaweza ukawa na profession yoyote lakini ukatafuta skills.
Sasa formula ya kuincrease value hii hapa.
Chukua TALENT yako (mf. Ubunifu mavazi)
Kisha ongeza UJUZI/SKILL katika Content Creation & Digital Marketing.
Alafu changanya na PROFESSION ya Public Relations.
Kaa pale angalia matokeo yake. And also you can imagine as well.
Kwahiyo, Dunia ya leo, ukijitafuta pande zote ukajipata wewe unakuwa mtu wa Gharama sana.
Narudia...
Sekondari niliosomea UMEME, na nimefanya wiring nyumba mpya ya Mzee wangu.
Chuo ndo Computer Engineering.
Kazini, nimejifunza MARKETING and I'm very COMPETENT on it.
Mtandaoni hususan TWITTER nimejifunza SELLING & CLOSING kupitia @NyandaAmosi na kitabu chake cha #Mgodi. Na kimenipa bonus nikiwa kazini. (Sipromote lkn maua yake apewe)
This is my definition, Skill is an ABILITY of changing normal thing to be UNIQUE & CREATIVE
Hizi ni baadhi ya skills:-
1. Graphics Design
2. Content Creation
3. Deal Closing
4. Website design
5. Digital Marketing
6. Tease and Ads Creations
WACHA KUZUNGUKA NA BAHASHA, JITAFUTE MUDA HAUKUSUBIRI!!

Loading suggestions...