Niliamka saa 11am siku hiyo, nikaingia bathroom nikafanya usafi wa mwili namaanisha kuoga ,piga mswaki n.k...baada ya kutoka kuoga nikapiga pamba zangu nikachukua perfume,ile kutikisa dah perfume ilikua imeisha nikasema kimoyomoyo sio swala nitawasiliana na @mozu245 anifosie....
Nikatoka Ghetto kuelekea kituo cha dalala ambacho kipo km 2 kutoka ninapoishi.
Nikiwa njiani na wenge langu la usingizi nikawa namuona mtu lakini kama simuelewi, Alikua anaenda hatua mbili alafu anasimama ananitazama π nikaingia upepo kidogoπ maana Arusha ni mkoa unaotisha..
Nikiwa njiani na wenge langu la usingizi nikawa namuona mtu lakini kama simuelewi, Alikua anaenda hatua mbili alafu anasimama ananitazama π nikaingia upepo kidogoπ maana Arusha ni mkoa unaotisha..
Lakini nilijikaza kisabuni na kuendelea kupiga hatua.
Niliendelea kupiga hatua,Na haikuchukua muda nikamkuta mtu yule.
Ebwanaa eh! Kumbe alikua ni mwanamke.
Lakini nikawa najiuliza π€ mrembo huyu na hii asubuhi ya saa 12 kasoro anatoka wapi na anaenda wapi? au ni jiniπ....
Niliendelea kupiga hatua,Na haikuchukua muda nikamkuta mtu yule.
Ebwanaa eh! Kumbe alikua ni mwanamke.
Lakini nikawa najiuliza π€ mrembo huyu na hii asubuhi ya saa 12 kasoro anatoka wapi na anaenda wapi? au ni jiniπ....
...Mara akasimama na kunigeukia "Mambo" akanisalimia na hapo nikazidi kuchanganyikiwa kutokana na sauti ile niloiskia kwa mwanadada yule.."poa za kwako" nikamjibu na kumuuliza huku tukiendelea kutembea Ado Ado...."me niko poa, we ni mwenyeji wa huku" akajibu na kuniuliza swali..
..."ndio me nimwenyeji wa huku" nikamjibu..."afadhali nimepata mwenyeji maana nlikua naogopa" akasema dada yule...."kwani ulikua unaelekea wapi?" nikamuuliza. akanijibu.."kituo cha daladala"
Nikamuuliza.."Na huku unatokea wapi" huku nikigeuza shingo yangu kumtazama....
Nikamuuliza.."Na huku unatokea wapi" huku nikigeuza shingo yangu kumtazama....
...nae akageuka na kunitazama π...Ebwanaa eeeeh! Nilikua sijui kama ni mzuri vile kutokana na kagiza, Uzuri wake ukaanza kunipa mashaka huenda nilikua sahihi labda ni Jini kweli... "Natoka kwa rafiki yangu Miriam" alinijibu..."Miriamu?" Nilimuuliza huku nikizidi kumtazama...
.."Ndio, unamjua?" alinijibu na kuniuliza swali..."kwa maeneo ya huku kuna Miriam mmoja tu! Ni mwanafunzi wa chuo" nilimjibu.."ndo huyo huyo me nimwanafunzi mwenzake...unajua watu wa mtaani kwako hadi raha jaman" aliniambia huku akiniangushia tabasam moja matata sanaaaπ.....
...ilinichukua sekunde 40 kuzinduka kutoka kwenye bumbuwazi nilolipata kutokana na lile tabasamu la mdada yule ambae sikua nimemuuliza hata jina..."aaah hapana siwajui sana maana me ni mtu wa mishe mishe lakini Miriam anakaa nyumba ya tatu kutoka ninapo ishi" nilimjibu ingawa...
...Ingawa nilimdanganya sikumuambia kua huyo rafiki yake Miriam ni ex wangu π sikutaka kupoteza bahati kizembe π.."Jina lako nani?" Yule dada aliniuliza...nilitaka nimtajie Tosha lakini nikakumbuka Tosha ndo jina analolijua Miriam ataniharibia akihadithiwa kuhusu me ππ....
..."Naitwa Moudy" Nilimjibu.."Nice to meet you Moudy" aliniambia huku akinipa mkono..."me too" Tukapeana mikono π€πΌ. Ebwanaa eeeeh! Huyo mtoto alikua wa aina yake kitendo cha kumpa mkono nikaanza kuwaza mbali ati tuko kwa Garden tunakimbizana kama wahindiπ....
..nilitolewa kwenye mawazo yale kwa swali aloniuliza "Mbona huulizi mimi naitwa nani au hutaki kunijua?"...."Hapana so hivyo nilitaka kukuliza lakini umeniwahi..unaitwa nani?" Kabla hajanijibu mara honi na sauti kavu ikaskika "Oyaaaaah! Kaka mkubwa na shemeji mnaendaa?"...
Kumbe tulishafika kituo cha daladala..."Tuwahi kwanza siti" ile pisi iliniambia huku ikinivuta mkono mpaka kwenye gariπ. hakika mbuzi kafia kwa muuza supuπ...tukapata siti pacha tukakaa p1 "Moudy me naitw..." kabla hajamalizia mara yule konda akatokea tena akiwa na mtoto...
.."Samahani shemeji, najua uko na Kakaa lakini naomba unisaidie kumpakata huyu mtoto mama yake atasimama" alisema yule konda huku akimkabidhi ile pisi mtoto "Dada njoo ukae tu hapa" niliongea huku nikisimama kumpisha dada yule ambae alikua ndo mwenye mtoto.....
....daladala ikachomoka ikiwa nyomi na wengi tukiwa tumesima, hapo ilikua ni mchanganyo wa perfume na jasho...wengine walinukia baby care π wengine perfume,wengine hatukunukia chochote wengine walinuka jasho japo ni Asubuhi ππ kama mnavyojua Hali ya kwenye daladala....
..konda alitangaza kituo wengi wakasema "shusha" huku me nikiwa napiga dua ile pisi isishuke kabla yanguπ..daladala ikasimama watu wakapungua ikawa tumesimama watu wachache na chakushukuru ile pisi haikushuka π€ ingawa bado nilikua na mashaka inaweza shuka mda wowote....
.."konda niache apo kilombero" iliskika sauti ya mdada..nikachungulia nikagundua ni yule nilomwachia siti ...alivyo amka tu nikawahi kukaa tena na ile pisi π..."Moudy niandike namba zako nitakutafuta maana nashuka posta" ilisema ile pisi huku ikitoa PIN kwenye simu yake ...
.."Sawa" nilimjibu nakuchukua ile simu na kuanza kuandika namba kwa umakini wa hali ya juu ili nisikosee nambaπ maana posta ni kituo kinachofata "isevu kabisa Moudy maana sina salio la kupiga"...."oooh! Hili gundu gani tena" nilijisemea kimoyo moyo na kujaribu kujipigia....
Kweli hakua na salio na kwa wakati ule hapakuwa na huduma ya ku beep kama sasa...nilimkabidhi simu yake huku nikizitazama namba mara mbili mbili mpaka alipo ipokea mwenyew π "konda niache posta" ilisema ile pis huku ikiamka nami nikaipisha nakumuambia "nauli usitoe ntalipia"..
"Haya sawa, Asanteh!" Ilinijibu huku ikiniacha na tabasamu moja matata "Bye" iliniaga na kushuka kwenye kwenye daladala baada ya kusimama...alimpa konda maelekezo kua nauli yako atalipa yule Kaka yako...konda hakua na neno kwasababu aliona tukiwa pamoja kipindi tunapanda....
....daladala ilisepa sasa ilikua inakaribia kituo cha mwisho kinachoitwa chini ya mti ...konda akaanza kukusanya Nauli yake, Alipo fika kwangu akasema "kaka! shemeji kasema utamlipia" nikamjibu "ndio" huku nikitoa wallet lakini nikakumbuka nina noti ya 5k kwenye mfuko wa shirt..
..nikamkabidhi konda nauli yake ..."chenchi hii apa kaka, alafu kaka nikusifu tu shemeji sio haba". Aisema konda.."hahaha" nikacheka alaf nikajipa maujiko na kumwambia "kawaida tu kaka" ππ "Kakaa ile ni level ya Range sio daladala, tafuta hela kakaa" konda alisema....
..huku akiendelea kukusanya nauli siti za nyuma ingawa yale maneno yaliniingia nikajisemea kimoyomoyo "kumpata mwanamke sio kazi kubwa lakini pesa ndo itafanya umbakishe kwako maana hatokula u handsome" nilishtuka kutoka kwenye mawazo yale baada ya brake kali ....
.."oya we dereva hujabeba mimba banaa, umebeba roho za watu kua makini na brake zako" iliskika sauti ya kijana mmoja kutoka siti ya nyuma akiwa amechafukwa na Rohoπ. Lakini ilikua tumekwisha fika kituo cha mwisho . Nilishuka na kuingia kwenye harakati zangu za kila siku....β
..Nikawa nafanya shughuli zangu lakini nikirelax kidogo natazama simu unajua kwa nini??π nilikua natazama kama yule mwanamke atakua amenitafutaπ.
Unataka kujua kama yule mwanamke alinitafuta??
Je!Tsh 500 iliniponzaje?
Basi usikose sehemu inayofata βπΏ.
#ITAENDELEA....
Unataka kujua kama yule mwanamke alinitafuta??
Je!Tsh 500 iliniponzaje?
Basi usikose sehemu inayofata βπΏ.
#ITAENDELEA....
Loading suggestions...