24 Tweets 52 reads May 03, 2023
Baada ya kumaliza siku, nikirudi nyumbani ni kuoga, kupata chakula na kuangalia taarifa ya habari kisha kusoma kidogo then kulala.
Jioni hii nikiwa naangalia taarifa ya habari mara naona taarifa ya mwanamke mmoja aliyeuwawa kikatili sana.
There's bad news..
Ila nikagundua..πŸ‘‡
Mwanamke anayetajwa kuuwawa alizungumziwa kwa sifa ya tofauti.
Jirani mmoja alisema.
"Niliambiwa kuna tukio la mauhaji kwenye haya majengo, haraka nikakimbia kuja hapa, nilipofika hapa nilikutana na mwili wa mwanamke ukiwa umekatwa katwa"
Taarifa hii ikachukua umakini wanguπŸ‘‡
Jirani aliendelea kusema..
"Sikuwa pekeangu tuliogopa ila kiubinadamu tulitaka kujua yule mtu ni mzima au amekufa, ikiwa nimzima apatiwe huduma ya Kwanza, katika kumkagua tukagundua mkono wake mmoja haupo na mwingine una vidole pungufu"
What cruelty is this..πŸ‘‡
Jirani aliendelea tena kusema..
"Baada ya kuona hana mkono, wengine walisema mkono upo kwenye chumba kingine huko, nikweli tukauona na hapo ndio tukajua tukio hili ni kubwa na lazima liwafikie polisi na tulifaanya ivyo"
Jirani huyu aliishia hapo..
Habari hii ilinifanyaπŸ‘‡
nijiulize maswali lakini nikakumbuka lile jina
Kama nimewahi kulisika sehemu ila sikuzipa umuhimu kumbukumbu hizo.
kingine nilichokuja kugundua ni kwambaπŸ‘‡
tukio lile lilifanyika majira ya usiku mnene na kugundulika asubuhi, inamaana hii habari niliiangalia masaa 21 mbele.
Sijakaa vizuri mara simu yangu iliita.
Ni jamaa yangu alinipigia simu na kuniambia..
"Unamkumbuka yule demu msagaji ninayekupaga story zake ameuwawa,πŸ‘‡
Baada ya mazungumzo na jamaa ndio nikaanza kukumbuka matukio ya miaka kadhaa nyuma.
Mwaka 2015 ni kati ya miaka ambayo nilikuwa najitafuta na katika kujitafuta nikajikuta nimedondokea kwenye upigaji picha, lakini vyuma bado vilikaza mbayaa.
Jamaa yangu aliwahi kuniambiaπŸ‘‡
twende Geita kwenye machimbo tukajaribu maisha huko.
Nilikataa sikwenda nikamjibu.
"We nenda tu "
Jamaa alienda Geita, alikaa mwaka mmoja then akarudi.
Alivyo rudi akaanza kunipigia story, kuna watu wanadondokewa na vifusi huko, next story niliona ananipanga kwambaπŸ‘‡
huko Geita aliwahi kupata demu pisi kali sana, sasa kuna demu mmoja msagaji ana pesa chafu huyo demu amemchukulia demu wake.πŸ˜‰
Story haikuniingia akilini, Absolutely nikajua mwana ananipiga kamba.
Yaani mwanamke kamuibia mwanamke wake..😁
Nikamwambia kausha
Sasa ilipofikaπŸ‘‡
2017 kuna video ilivuja ikimuonyesha mwanamke mmoja akimla mate mwanamke mwenzie na kumvisha pete.
Tukio lile likaniwazisha..
Mara nikaona taarifa kwenye mitandao.
"Mwanza: Wanawake waliovishana pete ya uchumba wafikishwa mahakama kuu leo"
Nikaona hili jambo liko seriousπŸ‘‡
nikalipa umakini.
Yule Jamaa yangu akanipigia simu tena akiniambia Yule demu aliyemchukuliga demu wake ndio huyo aliyekamatwa kwenye hilo tukio.
Hapa sasa nilianza kumuamini jamaa before nilihisi kamba😁
Jamaa akaendelea kusisitiza huyo mwanamke anapesa ndefu wee msikie tu.πŸ‘‡
Siku kadhaa mbele
Mahakama ikawaachia watuhumiwa kimya kimya tofauti na walivyo wakamata mpaka kwenye vyombo vya habari.
Perhaps kisheria hawakuwa na makosa
But..
Nikapata kiu ya kutaka kujua huyu mwanamke anayesemwa kuwa msagaji ni naniπŸ‘‡
Za chini chini nilizipata kuwa yule mwanamke aliyekuwa akivishwa pete ni mdogo wa kiongozi mmoja jina kapuni.
Na huyu mwanamke msagaji alikuwa anaitwa MILEMBE SULEIMAN ni Afisa ugavi wa kampuni ya madini ya dhahabu ya "Geita Gold Mine -GGM-"
Milembe alikuwaπŸ‘‡
Na pesa, alinunua magari mapya kila mara na hata alipoenda kununua gari yeye alitaja aina ya gari, iwe milioni mia, mia5, mia2 pesa yoyote alilipia bila kuomba huruma.
Mikato yake pensi kali raba kali miwani, ana tattoo on her left hand.
Akitembea anakaza like mwanaumeπŸ‘‡
Alipenda wanawake wenzie, alikuwa akitaka mwanamke alitumia gharama yoyote kumpata.
Hakuna pisi kali iliyochomoka kwake, uwe bishoo, kiongozi, mwanafunzi wa chuo.
Milembe akimuelewa demu wako anamchukua na Hakuna kitu utamfanya,
Alienda mbali zaidi mpaka kwenye wake za watuπŸ‘‡
Aligawa magari, nyumba chochote kile alitoa.
Akiingia club alget demu yeyote, kidume mwenye mpenzi wako ulipaswa kukaa umsikilize mjumbe anasema nini.
Utaulizwa unahitaji kitu gani ili uiachie hiyo pisi hapo, if ukitaka pesa utapewa na ukiwa mjeuri itachukuliwa kinguvu.πŸ‘‡
Akiwa ametoka kula bata na kuku kwa mrija na yuko hotel amepumzika, Milembe usiku huu anapokea simu inayomtaka aende mitaa ambayo alikuwa anafanya ujenzi wa nyumba zake.
Simu hiyo ilimwambia ni dharura ni muhimu na anapaswa kufika.πŸ‘‡
Milembe alifika eneo hilo la ujenzi wa nyumba zake lakini hakujua mahali hapo panaenda kuwa ni sehemu ya mwisho kukanyaga katika maisha yake.
Aliuwawa hapo, na inaonekana alianza kufanyiwa unyama huo katika chumba kimoja.
Baada ya hapo akatolewa na kwenda aneo lingine la πŸ‘‡
nyumba hizo akiendela kufanyiwa alichofanyiwa, na hapo ndipo umauti ukamkuta.
Asabuhi kunapambazuka Watoto wa majirani waliopenda kucheza pembeni mwa nyumba hizo, waliuona mwili huo na kwenda kuwapa taarifa wazazi.
Majirani walikuja na kukuta tayari MILEMBE SULEIMANπŸ‘‡
akiwa amefariki.
Amefariki katika Nyumba zake ambazo alikuwa akizijenga, Nyumba hizo zilifikia hatua ya kupauliwa.
Binafsi najiuliza aliwezaje kwenda hapo ikiwa mwenyewe.? Au aliambiwa maneno gani katika simu mpaka naye akatii amri hiyo.πŸ‘‡
MILEMBE si mpenzi wa mavazi ya kike lakini siku amefariki alikutwa amevaa kijora.
Jambo ambalo liliwashangaza hata majirani, kwani enzi za uhai wa milembe hawakuwahi Kumuona akiwa kwenye vazi hilo la kijora.
Lakini wakati anakuja hapo, usafiri aliokuja nao alipaki wapiπŸ‘‡
nakama alikodi usafiri ana gari zake why atumie usafiri wa kukodi.
Na wakati anafanyiwa ukatili huo hakupiga kelele majirani hawakuhisi chochote.
Aliyepiga simu..πŸ™Œ
Baada ya tukio hilo waajiri wake wakachapisha taarifa kwa kumtambua milembe kama mwanaume,
Why?.. πŸ‘‡
But kuna nyingine tena ikachapishwa ambayo ilionekana iko sahihi.
Hatujui pengine baada ya kuchapisha ya Mwanzo wakakosolewa na wakaamua kubadilisha or watu wanaopenda kwenda na upepo waliamua kuediti ili watujaze mjini pachangamke.πŸ‘‡
SahihiπŸ‘‡. Si hahihiπŸ‘‡
Tutajiuliza maswali mengi ya kufikirisha but yanatosha, kazi tuwaachie polisi..
Huyu ndiye MILEMBE SULEIMAN
Stay safe kwa ground mambo ni mengi sana.πŸ™
Usiache kunifollow as @wisdomjaykwa #wisdomjaykwa

Loading suggestions...