Sistiinho
Sistiinho

@sistiinho

15 Tweets 1 reads May 21, 2023
#uzi wa mbinu | Rulani Mokwena
Na @sistiinho
Mamelod Sundowns wanatajwa kuwa klabu tishio zaidi barani Afrika, wamebeba ubingwa wa ligi kuu Afrika kusini na sasa wametanguliza mguu moja kwenye nusu fainali ya #CafCL baada ya kushinda magoli 4-1 ugenini kwa CR Belouizdad
Leo nimekuandalia machache niliyong'amua kwenye #KitabuChaMbinu cha kocha Rulani Mokwena kuzingatia;
๐Ÿ‘‰mfumo
๐Ÿ‘‰kikosi
๐Ÿ‘‰staili ya uchezaji (wakiwa na wasipokua mpira)
MFUMO
๐Ÿ‘๏ธ Mifumo wanayotumia ni 4-3-3,4-4-2 na 3-4-3
๐Ÿ‘๏ธKikosi ๐Ÿ‘‰Kipa - Ronwen Williams ๐Ÿ‘‰Mabeki - Khuluso Mudau, Grant Kekana, Mothobi Mvala na Mophisa Modiba ๐Ÿ‘‰Viungo - Teboho Mokoena, Neo Maema na Marcelo Allende ๐Ÿ‘‰ Washambuliaji - Themba Zwane, Peter Shalulile na Casius Mailula
๐Ÿ‘๏ธWakiwa na mpira
๐Ÿ‘‰ Kwenye mfumo wa 4-4-2 wenye muundo wa diamond ambapo muundo huu hubadilika eneo la mbele kutoka kwenye 4-3-3 kwa nahodha Themba Zwane kushuka eneo la kiungo mbele ya Single pivot ya Mokoena,Maema na Allende na kuwaacha Shalulile na Mailula mstari wa mbele
๐Ÿ‘‰ Wakijenga shambulizi huwa kwenye muundo wa 3-3-3-2, kwa kipa wao Williams kuwa kwenye mstari mmoja na mabeki wa kati Kekana na Mvala, huku mabeki wa pembeni, Mudau na Modiba wakiwa kwenye mstari wa kiungo usawa wa Kekana na kufanikiwa kuvuka presha ya wapinzani
๐Ÿ‘‰ Uendelezaji wa shambulizi huhusisha viungo wa washambuliaji, Maema na Allende ambao husimama nyuma ya mstari wa pili wa uzuiaji wa wapinzani kupokea pasi kutoka kwa Mokoena,Mudau na Modiba
๐Ÿ‘‰ Upenyaji na Utengenezaji wa nafasi hutegemea muunganiko kati ya Allende,Maema na Zwane ambaye hushuka eneo la katikati kuongeza idadi na kuwazidi wapinzani (Overload)
๐Ÿ‘‰Kama wapinzani watakua wamerudi nyuma kuzuia kwenye theluthi yao ya uzuiaji (low&block) Modiba na Mudau hushambulia mapana ya uwanja kutanua uwanja ili shape ya uzuiaji itanuke kutengeneza mianya katikati ya mistari
๐Ÿ‘‰ Umaliziaji wa nafasi hutegemea washambuliaji wao Shalulile na Mailula kushambulia nafasi nyuma ya mabeki wa wapinzani ambao huvurugika kwa mikimbio ya Zwane na wao kushambulia nusu nafasi
๐Ÿ‘๏ธ Wasipokua na mpira
๐Ÿ‘‰Hushinikiza kuanzia mbele kwa kuzuia nafasi zaidi (space oriented pressing) wakiwa kwenye muundo wa 4-4-2, Shalulile na Mailula waki-press, Zwane huzuia mpira kupita kwa Kiungo wa kati wa wapinzani
๐Ÿ‘‰ Wapinzani wakivuka hadi theluthi ya kati na nyuma, huzuia kwenye muundo wa 4-3-3, Zwane huwa sambamba na Shalulile na Mailula kwenye mstari wa mbele wa uzuiaji
๐Ÿ‘‰Allende na Maema huwa sambamba na Mokoena huku wakiwa wapo pamoja na hawajaachiana nafasi kubwa kati ya mtu na mtu kuzuia wapinzani kupita eneo la kati
๐Ÿ‘‰Pia kama wapinzani watapita pembeni Allende na Maema huwasaidia Mudau na Modiba wasiweze kutengenezewa situation ya 2v1

Loading suggestions...