Creative Vans πŸ’Ά
Creative Vans πŸ’Ά

@creative_vans

16 Tweets 127 reads Mar 17, 2023
Kama Wewe Ni MFANYABIASHARA.. Soma Hii
.
Ep 02
.
Jinsi ya Kutengeneza Poster Kali Ya Duka La Nguo Kwa Kutumia Canva Kwenye Simu au PC
.
Hata kama haujawahi tumia Canva, Baada Ya Kusoma Huu Uzi Nakuhakikishia Kwamba Utaweza ...
.
[ TWENDE PAMOJA ] πŸ‘‡
Kabla hatujaenda mbali..Kama unapenda Kuendelea Kupata Content Kama Hizi, Nisaidie Kulike na Kuretweet Iwafikie Wengi Wanaopenda Pia..
Hatua ya kwanza kabisa kabla hata haujafungua Canva, Hakikisha unajua mlengwa wa Tangazo lako.. ili ujumbe uendane na kile anachohitaji ili kutatua shida aliyonayo...
Embu fikiria hata wewe unaumwa kichwa afu linatokea Tangazo la panadol wanasema "Vidonge hivi vina muundo mzuri" πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… Haina maana si ndio??? πŸ‘‡
Sasa umeshajua umuhimu Wa ujumbe wako... Unaweza jifunza kuandika ujumbe unaovutia wateja Kwa kusoma Copywriting BURE Google & YouTube (Kiingereza ) Au Kwa @NyandaAmosi (Kiswahili)
Haya Tuendelee na Canva Sasa πŸ‘‡
Fungua app Ya Canva, Bonyeza alama ya "+" ili Kutengeneza kazi mpya.....
Chagua "Custom size" ... Urefu Kwa Upana weka "1080 * 1080" Px...
Bonyeza "Create Design"..... TWENDE KAZIπŸ‘‡
Hizi hapa chini ndo material tutakazo tumia Kwa Ajili ya Kutengeneza Poster Yetu.... Tumia hayo majina kuzipata kama hiziπŸ‘‡
Utaanza Kwa kuweka rectangle ya blue πŸ”΅ ... Ikuze iwe kubwa ijae kwenye frame nzima ili iwe kama background.....
Pili chukua iyo "Pattern Background" iweke apo... Chagua rangi nyeupe afu "Transparency" weka 5-10% Tu inatosha...
Ipige Loki πŸ”’..ili isikusumbue
Afu Kwa chini malizia Kwa kuweka "Rectangle" nyeupe.. Utapata mwonekano kama huu hapa chiniπŸ‘‡
Sasa weka "Frame" kisha zipange ziwe 4 Kwa mpangilio Kama huu hapa chini...
Hizi tutatumia kuweka picha zetu Kwa mpangilio unaovutia πŸ‘‡
Haya sasa chukua zile Picha, Mojamoja ivute katikati ya izo "Frame" zitajipachika zenyewe.. Kurekebisha ukubwa au kuisogeza picha ya ndani ya frame.. ibonyeze picha mara mbili
Picha ya "Jeans" iweke Tu Kwa chini pembeni bila Kutumia frame πŸ‘‡
Kwa Ajili ya kuitambulisha biashara yako, Weka Logo yako... Social medi Icons hicho kimstari hapo upande Wa kushoto πŸ‘‡
Mwisho Kabisa, Weka Maneno yako Kwa kuanza na Kichwa cha Tangazo, Ujumbe. Na Contact Zako...
Font nimetumia "Poppins" na "Balloon Small Caps Extra"
Hongera Sana Kwa Kufikia Hatua Hii.. πŸ₯³πŸ₯³πŸ₯³πŸ₯³
Sasa unaweza design poster kama hii kwa Ajili ya Biashara yako πŸ‘‡
#CanvaPro #canvatz @canva
Kama Unatamani kuona post inayofuata kuhusu Canva Design... Hakikisha Umenifollow, Like na Kuretweet hii post
Pitia post iliyopita πŸ‘‡

Loading suggestions...