Digital Nomad ( YT @mafolebaraka)
Digital Nomad ( YT @mafolebaraka)

@mafolebaraka

8 Tweets Apr 08, 2023
Jana nilialikwa na @AfroSheFound pamoja na @jukwaaafrica kuzungumza kuhusu kazi za Remote.
Na hii ni thread ndefu ya nilichokizungumza.
Shuka nayo
Remote working ni mfumo wa ufanyaji kazi unaomruhusu mfanyakazi kufanya kazi nje ya eneo la ofisi.
Wafanyakazi wengi wa remote hupendelea kufanya kazi kwenye maeneo ya fukwe ama migahawa.
Maeneo ya kupata kazi za remote ni pamoja na
1.Majukwaa ya Freelancing
Majukwaa haya ni maalum kwa ajili ya watu wanaotafuta kazi za kidijiti za muda mfupi na mrefu.
Moja ya majukwaa ya maarufu ya freelancing ni pamoja na Upwork, Guru, Fiverr, Peopleperhour na Gigspace.
2.Mitandao ya kijamii
Hii ni moja ya eneo ambalo kazi nyingi za kidijitali hutangazwa.
Moja ya mitandao maarufu kwa ajili ya kupata kazi za remote ni pamoja na Linkedin na Twitter.
AD: Kongole kwa @WomenFund_TZ , Miaka 15 ya kusapoti jitihada za wanawake wanaotetea haki za wanawake na mabinti si mchezo.
Mafanikio ni makubwa na hakika mnastahili pongezi kwa kazi kubwa mmefanya kwenye taifa hili
#Miaka15MfukowaWanawake
3. Events mbalimbali
Events hususani za Tech ni moja ya eneo la kuwapata wateja wa kazi za remote.
Moja ya events za Tanzania ambazo naweza kukushauri uende kusaka clients ni pamoja na Innovation week & Sahara Sparks.
4. Wafuate wateja walipo
Kuna muda hutakiwi kusubiri wateja wakutafute, amka, piga mswaki wafuate walipo.
Tuma emails kwa kampuni unayotaka kufanya nayo kazi, Tuma dm kwa client unaemtamani na mwisho piga simu kwa Mmiliki wa kampuni unayotaka kufanya kazi.
5.Majukwaa ya kazi za remote
Kuna tovuti kazi zake kubwa ni kuposti matangazo ya kazi za remote zilizopo kwa wakati husika.
Moja ya tovuti hizo ni pamoja na glassdoor, Crossover na Indeed.
Zichangamkie Mwaisa.

Loading suggestions...