BAD NUMBER🥷🏿
BAD NUMBER🥷🏿

@ByDurahRich

31 Tweets 1,209 reads Jan 23, 2023
KWANINI KITABU CHA HENOKO KILIFICHWA KISITUMIKE KWENYE INJILI?
SABABU HIZI👇
NJOO NIKUPE SIRI ZA UFUNUO WA HENOKO ILA IWE NI SIRI YAKO USIMWAMBIE MTU.
Miongoni mwa watu walioweka historia kubwa kwenye biblia ukiacha Yesu,ni watatu (ingawa Ni wawili... ambao hawakuonja mauti bali walitwaliwa,
yaani Eliya na Henoko) Musa nimemuweka kwa kuwa inaonekana alikufa
Lakini hakuna anayejua na mwili wake ulikuja kuonekana mbele za Mungu ukigombaniwa na shetani na malaika.
Sasa Musa tumesoma vitabu vyake vitano vinavyomhusu ingawa inaonekana ALIKUFA ila kaburi lake hakuna
anayejua ni Siri yao na Mungu na hakuna asiyefahamu habari zake ameandikwa sana kwenye vitabu vya wafalme
lkn ajabu ni kwamba wajanja walizuia na kuondoa historia ya Henoko ambapo Kuna kitabu chake kinaitwa UFUNIO WA HENOKO , waliondoa Lakini Mimi nataka nikupe madini machache.
Kinachochekesha Henoko tunaona habari zake kwenye Mwanzo 5:21-24
“Henoko akaishi miaka mia tatu sitini na mitano, akamzaa Methusela.
Henoko akaenda pamoja na Mungu, baada ya kumzaa Methusela miaka mia tatu, akazaa wana waume na wake. Siku zote za Henoko ni miaka mia tatu na mi5
sitini na mitano. Henoko akaenda pamoja na Mungu, naye akatoweka, maana Mungu Alimtwaa”
Halafu eti mtu aliyetembea na Mungu vizuri na akatwaliwa halafu asiwe na historia namna alivyokwenda na Mungu?
Ukisoma Waraka wa Yuda 1:14-16
Ndio utaona Kulikuwa na kitabu cha Henoko na Yuda amesoma Sana hiki kitabu anaposema
“Na Henoko mtu wa saba baada ya Adamu, aitoa maneno ya Unabii juu ya hao,
akisema, angalia Bwana alikuja na watakatifu wake, maelfu, maelfu, ili afanye hukumu
juu ya watu wote na kuwaadhibisha wote, wasiomcha Mungu, kwa ajili ya kazi zao zote za upotevu walizozitenda,
bila kumcha Mungu, na kwa ajili ya maneno magumu yote, ambayo hao wenye dhambi,
wasiomcha Mungu wameyanena juu yake. Watu hawa ni wenye kunung’unika wenye kulalamika,
waendao kwa tama zao, na vinywa vyao vyanena maneno makuu mno ya kiburi, wakipendelea watu wenye cheo kwa ajili ya faida”.
Hii inaonyesha kabisa mtume Yuda amenukuu maneno ya Henoko toka kwenye ufunuo wa henoko lkn wajanja wakautoa.....lkn subiri nikupe Siri
Ufunuo wa Henoko
Aliouona Alipo pelekwa Mbinguni Chini Ya Usimamizi Wa Malaika Uriel.
Henoko alipokea maneno ya unabii kutoka mbinguni kwa Mungu Aliye Hai, na kufunuliwa kupitia usimamizi wa malaika mkalimani aitwaye;
URIEL. Malaika Uriel ndiye aliyemtembeza Henoko katika ulimwengu wa roho,
na kumtembeza mbinguni, kuzimu na maeneo yote ya ulimwengu wa roho.....
na inaonyesha huyu ndiye malaika aliyemsimamia mtume Yohana katika ufunuo wake alioonyeshwa na Yesu.
Henoko alienda na Mungu Aliye Hai, na kutumika katika matendo makuu sana miujiza na ajabu kuu sana.
Alifunuliwa siri kuu sana za mbinguni.
Lakini waandishi wa biblia, SEPTUAGINTA kutoka Ugiriki, chini ya usimamizi wa waamini wa hapo awali na Waprotestanti waliamua
KUVIONDOA VITABU VINGI VYA BIBLIA NA KUKATAA VISIANDIKWE MAANA WALIONA aibu sana kutokana na MAMBO MACHAFU
WALIYOYAFANYA MALAIKA WAASI KUTOKA MBINGUNI NA HENOKO ALIYAWEKA WAZI HAYO MAMBO MACHAFU Mwanzo 6:1-5.
Ukisoma kitabu maalumu cha Henoko 7:1 pana siri nyingi sana alizofunuliwa na Mungu Aliye Hai chini ya usimamizi wa malaika URIEL, KAMA MALAIKA MKALIMANI yaani
anaye tafsiri na kufundisha; Ayubu 33:14-24, Waebrania 1:13-14.
UFUNUO ALIOUONA HENOKO JUU YA MALAIKA WAITWAO; WANA WA MUNGU NA KAZI ZAO;
1. Henoko alifunuliwa kazi mbalimbali na utendaji wa aina hii ya malaika waitwao; Wana wa Mungu.
2. Malaika waitwao wana wa Mungu waliwafundisha wanadamu wakati huo namna ya kutengeneza silaha za aina mbalimbali.....silaha zote unazoziona duniani America,urusi,Korea,ktk falme za kiarabu, Israel, sio Mungu aliyewapa ujuzi wa kutengeneza Bali Ni hawa malaika waasi......
ndio maana leo Kuna watu mnadhani Wana akili kubwa sana lkn si akili ya MUNGU, Mungu ni wa mipaka alimpa mwanadamu mipaka.
Ndio waliowafundisha wanadamu mapenzi ya jinsia moja,kulawitiana,kusagana…
chanzo kikuu ni nchi za magharibi ambako Kuna mbegu nyingi Sana za malaika waasi.
3. Malaika Azazel, ambaye ndiye aliyekuwa kamanda mkuu wa kikosi hiki cha malaika waitwao; WANA WA MUNGU, kuwazuia malaika wenzake kutenda ushenzi na uchafu wa kutisha,
kwa kufanya ngono na wanadamu, Mwanzo 6:1-7 na Dunia ikaharibika.
Ndio maana kwa kuona aibu wataalamu na watafiti wa maandiko matakatifu (Biblia)
waliamua Kitabu hiki kiondolewe kisiwekwe pamoja na vitabu vingine vya Biblia Takatifu. Uovu huu na uchafu huu uliendelea
kwa siku kadhaa na kuharibu kusudi la Mungu Aliye Hai
4. Baadhi ya malaika waaminifu, katika kundi liitwalo WANA WA MUNGU, walirudi mbinguni na kumweleza Mungu juu ya uchafu wa ngono ulifanywa na malaika wenzao hapa Duniani.==
ndipo wale malaika waharibifu walioasi na kufanya ngono na kuwaoa wanadamu, kinyume na sheria ya
Mungu inavyowataka, walikamatwa na kufungwa ktk gereza kuu lililochini sana ya Dunia. Soma Yuda 1:6 ndie pekee aliyetoa hii siri maana alisoma Sana kitabu hiki cha henoko.
Anasema
Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu.
5. Malaika kiongozi wa wana wa Mungu, alienda mbinguni kumwomba Mungu BABA awasamehe wana wa Mungu
(malaika walioasi), lakini Mungu Alikataa, maana mbingu zilipata aibu kubwa sana.
Ndio maana wakati wa mtume Paulo, wamama waliambiwa wafunike vichwa kwa ajili ya malaika.
Lengo ilikuwa ni kuwazuia malaika wasijaribiwe tena kwa kuwatamani wanawake na kuwaka tama. 1Kor 11:10
“ Kwahiyo imempasa mwanamke awe na dalili ya kumilikiwa kichwani, kwa ajili ya malaika, ukitazama katika biblia Takatifu, Nukuu ya 1Kor 11:10, inaelekeza ;
Mwanzo 6:2, kama andiko ambatanishi na linalosindikiza habari hii.
6. Baada ya malaika waitwao wana wa Mungu kuzaa na wanadamu, walizaliwa wanadamu wenye urefu wa zaidi ya futi; 20, yaani Majitu==
Mfano; wanefili, wana wa Anak, na Warefai. Mungu Alimweleza Henoko kwa kirefu sana juu ya gharika ya Nuru na jinsi itakavyokuwa. Henoko 7:1
7. Baadhi ya Wanefili walisalimika katika gharika ya Nuhu, ndio maana wakati wa kuiteka Yeriko wapelelezi wa Yoshua walileta taarifa ya wanefili (majitu)
na jinsi wao walivyojiona kama panzi mbele yao. Wakati wa Daudi Aliinuka Goliathi moja ya majitu yanayotokana na ;
Malaika waitwao wana wa Mungu Kuzaa na wanadamu, aliwatisha sana Waisrael, hadi alipouawa na Daudi Kwa Ajabu ya Mungu Kupitia jiwe.
8. Honoko alikuwa Nabii wa kiwango cha juu sana. Alifunuliwa ; siri za mbinguni, siri za malaika, siri za wanadamu na siri za shetani. Aliona maono
mengi sana yaliwashangaza waumini wa kizazi cha awali. Baadhi ya waumini wa enzi hizo , walivutiwa sana na maneno aliyo yaona Henoko.
Wakawa na hamu ya kujua zaidi.
Japokuwa kitabu hiki kilizuiwa kisiwafikie watu ili kuficha ukweli na aibu ya kutisha ktk historia ya mbingu na
ukristo, Waprotestanti wakakipiga marufuku kitabu hiki na vinginevyo vya Biblia Takatifu.
Lakini hata sasa bado Kitabu cha Henoko kipo, kimetunzwa na kimehifadhiwa. Wanafunzi wa Biblia Wanaposoma na kufikia, kiwango cha juu hasa katika kujifunza kujua Asili na ufunuo wa mambo ya
Mungu Mtakatifu. MUNGU ANAMFUNULIA HENOKO MPANGO NA SIRI ZA SHETANI:=
Shetani alitoka mbinguni baada ya kufukuzwa, aliposhindwa vita, lakini alikuwa akijua mipango mingi sana na siri nyingi sana za Mungu
Akanza mkakati maalumu wa kuvurugua mipango ya Mungu.
Shetani kwa kuwatumia malaika wenzake waitwao;
wana wa Mungu, aliamua kuingilia mfumo wa damu za wanadamu kwa kuwashawishi malaika wafanye ngono na wanadamu.
Maana alijua Yesu Kristo atazaliwa Duniani ili kuwakomboa wanadamu na dhambi zao.
Shetani alijua malaika wakikutana kimwili na wanadamu itapelekea damu ya Yesu Kristo isiwe ya mwanadamu, bali ichanganyike na ile ya wanefili (majitu), Lakini shetani hakufanikiwa ktk mpango huu.
Shetani alikuwa anaufahamu mpango wa Mungu Kumpa Ibrahimu nchi ya Kanaani, akaamua kuiwahi ardhi hii na kuwaweka wanefili.....
wewe jiulize tu wanefili kwanini waliatamia sana Lakini nchi ya kanaani? Lakini hakufanikiwa katika hili.
#Beneh_Elohim
ni moja ya malaika kutoka kundi la wana wa Mungu ambao wamefungwa hivi sana akisubiri hukumu......kitabu hiki cha henoko kimeandika.
#Erakieli
ni moja ya malaika mwana wa Mungu aliyeasi ambae baada ya kuasi aliwafundisha wanadamu kufanya mazingaombwe...
huyu ndiye chanzo cha elimu yote ya mazingaombwe hapa duniani ambapo hata makanisani imeingia na watumishi baadhi matapeli huzitumia kufanya miujiza,
kuona matatizo ya watu Kama nanabii lkn Ni elimu ya Erakieli.
#Samiazaeli
ni moja ya malaika viongozi ktk wana wa Mungu ambaye aliwafundisha wanadamu uharibifu na uovu wa kutisha.
#Azazeli
ni malaika kiongozi ktk wana wa Mungu na muasi aliyewafundisha wanadamu;
mambo ya urembo,hizi make up zote za wanawake mwalimu wa hizo ni Azazeli....
ndiye aliwafundisha uchawi, silaha za kichawi, na kuwafundisha wanadamu kuwa wachawi na washirikina.
Alishirikiana na Rafaimu na Zanzuimu, baadaye, walikamatwa na wamefungwa na Mungu ktk Gereza kuu chini ya Dunia.
Jitahidi kunifuatilia au fuatilia ukipate hicho kitabu cha ufunuo wa henoko hutajuta kumfahamu kuhani.....japo ni gharama kubwa sana.
IKUMBUKWE MUNGU HAKUMUUMBA MWANADAMU AWE MUASI
(Rejea zote umepewa fanya tafiti ongezea na maarifa aliyokupa Mungu ndipo uje tubishane)
#MCHAPO
Twende taratibu mpaka siku tuelewane,

Loading suggestions...