Gillsant v10
Gillsant v10

@GillsaInt

18 Tweets 2 reads Feb 13, 2024
Niche Market: Kitu muhimu kijifunza ili ufanikiwe kirahisi kwenye biashara yoyote online au offline. Kabla sijaanza kuelezea Business Models moja moja ningependa tujifunze kuhusu Niche Markert leo. #UZI #MadiniYaGill
Makosa mawili ambayo wanafanya haswa wafanyabiashara wanaoanza ni kuanzisha biashara ambayo ina ushindani mkubwa na hawana njia yoyote ya kushindana mfano uanzishe biashara ya soda, ushindane na Coca Cola pia Kuuza bidhaa na zile zile ambazo watu wengine 4,325,978 wanauza.
Niche (niish or niich inategemea umesomea wapi) ni nini?– Sisi tutaiita “Kichaka” - Ni kundi maalum la wateja lenye mahitaji maalum ambalo mfanyabiashara anachagua ili aweze kutoa huduma au bidhaa kwao. Wataalam wengine wanaita (Market Segment).
Mifano ya Niche 
Badala ya kusema utawaauzia watu "wote" bidhaa zako. Jaribu kufanya hivi
Afya: 
Niche: Vyakula vya asili, virutubisho, vifaa vya mazoezi, wanaume wenye vitambi, dawa za chunusi kwa wanaume wenye ngozi zenye mafuta
Pesa: 
Niche: Andika kuhusu Crypto, Fundisha Forex, Jinsi ya kutengeneza pesa kupitia affiliate marketing, Betting, kutengeneza pesa kutumia youtube, 
Hobbies: 
Niche: Viatu vya Kukimbilia, Vifaa vya Music, Nguo za kuogela, Jezi za mpira, Jezi za Simba
Fashion: 
Niche: Nguo za watu wanene, viatu vya watu wenye miguu mikubwa, nguo za Watoto wa kike
Urembo: 
Niche: Mafuta ya ngozi ya asili, makeup za watu wenye ngozi nyeusi, mafuta ya nywele za asili
Technology: 
Niche: laptops kwa ajili ya games, Smart TV tu za Samsung
Vifaa vya nyumbani: 
Niche: Mapambo ya ndani, vifaa vya jikoni, vifaa vya bustanini, mashine ndogo zinazorahisisha mapishi, etc 
Magari: 
Niche: Spea za gari za kutoka UK tu, Fundi Range Rover tu, Radio za magari
Social Media Marketing: 
Niche: Kwa watu wenye shule tu, Jinsi ya kutumia tiktok kwenye biashara, Kufanya matangazo ya biashara instagram, 
Vyakula:
Niche: Chakula cha watu wenye kisukari, Vyakula vya kuongeza uzito, Utumbo na Miguu ya kuku tu, Jinsi ya kupika keki, Diet food
Kuna wakati unaweza kwenda na niche yako chini zaidi mfano: Duka la nguo za watoto wa kiume chini ya mwaka mmoja waishio Mwanza. 
Niche Ideas zipo nyingi sana Chakula, Mahusiano, Afya, Pesa, Technology and Urembo. Hizi ni baadhi ya niche ambazo zinaitwa Evergreen.
Iwe mvua au jua watu watahitaji hizi huduma. Kwa hio ukikosa niche idea unaweza komaa na moja wapo. 
Narrow Niche: Usije ukafanya kosa la kujibania michongo kwa kulenga kundi dogo kabisa mfano: Duka la mapazia ya kijani au Duka la chakula cha mbwa aina ya Norwegian Lundehund
Tofauti ya Niche “Kichaka” na Target Markert “Msitu” ni nini? 
Niche (Kichaka) ni kundi dogo la wateja lenye mahitaji maalum (Specific). Target market (Msitu) ni kundi kubwa linalojumuisha wateja wote wenye mahitaji mbali mbali.
Faida za Niche Marketing 
â—ľ Kupunguza ushindani
â—ľ Faida kubwa ya bidhaa
â—ľ Uaminifu kuongezeka
◾ Ni rahisi kuwafikia wateja wako kwa matangazo (Better Targeting) 
â—ľ Unawaelewa wateja wako na mahaitaji yao kwa urahisi
Tupate Wadhamini: Njaanuary! imekaba? Usikonde… Mcheki Uncle wako wa abroad mapemaaaa mwambie unaweza pokea pesa kwa Mpesa fastaaa na kwa usalama asihangaike.
Like, Comment na Retweet nipate nguvu ya kuwaletea mdini zaidi.
Jinsi ya kuchagua Niche 
â—ľ Wateja: Chagua kichaka (Niche) ambayo ina wateja wa kutosha kuweza kuanzisha bishara na ikapata faida.
â—ľ Uwezekano wa kupata faida nzuri: Fanya utafiti wa bei za ununuzi wa bidhaa au huduma unayotaka kutoa. Usiuze kitu ambacho hakikupi faida.
◾ Angalia wateja wako wanapata vikwazo gani au ni bidhaa gani hawapati na bishara yako itatatua vipi changamoto hizo. 
â—ľ Washindani: Fanya utafiti wa washindani wako angalia ni vitu gani hawafanyi na biashra yako inaweza kuvifanya. Unaweza angalia social media na website zao
Biashara yoyote unayotaka kuanzisha iwe ni duka lako la Instagram (ecom), dropshipping, dropservicing, influencer marketing, online course, affiliate marketing, kilimo, mangi shop, hakikisha kwanza umechagua kichaka chako na utaenda kutatua changamoto zao.
Angalizo: Ni muhimu kufahamu niche inaweza badilika baada ya muda kile ambacho kilikua kinakulipa sasa hivi kinaweza kisikulipe baada ya muda. Kwahio ni muhimu kutathmini mara kwa mara mbinu zako na kubadili inapobidi.
Follow page yangu kwa madini zaidi kila siku.
Kama umepata kitu kipya. RETWEET, Comment neno Madini, Weka 🔥 emoji na tag wana 3. #TutoboeWote

Loading suggestions...