15 Tweets 1,229 reads Sep 22, 2022
KAZI ZINAZOENDANA NA NYOTA YAKO...
PUNDA.
Kazi zinazowafaa ni Jeshi, Kazi za Uokoaji, Michezo, Uuzaji, Upasuaji, Kufundisha (Ualimu), Masuala ya Fedha. Biashara za kubadili fedha,Biasharaza kuuza vifaa vya michezo, biashara za vifaa vya shule au maduka ya madawa.
NG'OMBE...
muziki, kazi zinazohusiana na chakula, hoteli, migahawa, kazi za ujenzi, kazi za mashamba, kazi za uhasibu, na kazi za sanaa hasa uchoraji au uchongaji vinyago.
MAPACHA...
Kazi zao hasa ni zile zinazohusiana na mambo ya utangazaji wa Radio na Televisheni. Kazi ambazo zinahusika na mambo ya vitabu au uchapishaji vitabu. Kazi za kufundisha na kazi za ushauri nasaha.Vilevile wenye nyota hii wanatakiwa wafanye kazi za ukalimani au biashara
KAA..
Madaktari au Wauguzi, kazi za baharini kama vile mabaharia, kazi za huduma ya chakula kama hoteli, migahawa, kazi za kuhudumia watoto kama katika shule za chekechea, kazi za benki au kazi za maneja utumishi au kazi za kuandika
SIMBA...
kazi za usimamizi, kama katika kampuni yake binafsi au katika mashirika au biashara, kazi za michezo au uongozi wa michezo.Wanatakiwa wafanye kazi za usonara au kazi za kuuza au kutengeneza mavazi ya mitindo.Vilevile wanatakiwa wafanye kazi za uigizaji.
MASHUKE..
Kazi zao ni zile zinazohusiana na uchapishaji, utangazaji, afya, udaktari, kazi za unesi, kazi za uongozi, elimu na kufundisha, biashara yoyote.
Wanapenda Uhuru...Hawezi fanya kazi yoyote itakayomfanya ajihisi anabanwa.
BOFYA HAPO KAMA HUIJUI NYOTA YAKO...
MIZANI...
Wenye nyota hii kazi nzuri kwao huwa ni kazi za uhusiano wa jamii, Ushauri wa Ndoa, Biashara ya Sanaa, Ushauri wa Mambo ya Urembo, Uanasheria, Uhakimu pia biashara za kuziba pancha na kujaza upepo au kupamba maharusi zinawafaa zaidi
NGE...
Kazi zinazowafaa wenye nyota hii ni kazi za madawa au tiba, kazi za upelelezi, kazi za utafiti, kazi za fundi bomba, kazi za elimu ya kale, na kazi za ushauri wa mambo ya mapenzi na ngono au biashara zinazoendana na mambo hayo.
MSHALE...
Kazi zinazowafaa ni za usafiri, kazi za sheria, Wakili au Hakimu, kazi za uandishi, ualimu, dini, sheikh au padri au makanisani au misikitini, michezo, kazi za kijeshi na uuzaji.
MBUZI
Ni wenye kupenda utekelezaji wa kazi wa hali ya juu na wao wanapoagizwa hufanya hivyo.Kazi zao zinazowafaa ni zile za kutumia akili, Uhandisi, Usanifu Majengo, Saveya, kazi za Serikali, Siasa na Daktari wa Meno.
NDOO
Watu wa Ndoo ni wenye mawazo ya ubunifu na wenye kugundua njia mpya na zenye uhakika katika kazi.
Kazi zinazowafaa ni za uhandisi wa umeme, kompyuta, utafiti wa Sayansi, utabiri, huduma za jamii na utafiti wa mambo ya kale.
SAMAKI...
Kipaji cha kutafsiri mambo, huwasaidia vilvile kufanya kazi za sanaa kama vile kupiga picha na kazi za muziki au maigizo
Kazi zingine zinazowafaa ni za kuhudumia wagonjwa, kucheza shoo, uaskari wa majini (Navy) kazi za dini au kazi za kutoa ushauri nasaha (Counselling)
PS; Hizo sio kazi unazozipenda bali ni unazitakiwa kufanya kulingana na nyota yako.

Loading suggestions...