Dr. Mlaluko, MD
Dr. Mlaluko, MD

@drmlalukoMD

5 Tweets 172 reads Aug 23, 2022
#FAHAMU: NAMNA RAHISI YA KUMSAIDIA MTU ALIYEPALIWA NA CHAKULA/KINYWAJI
#UZI💥
Kupaliwa na hali inayotokana kitu (chakula, kinywaji n.k) kuingia katika njia ya hewa. Baadhi hupaliwa na hata mate. Kwa watoto huweza kupaliwa na maziwa.
DALILI
• Kukohoa sana,
• Kutapika (baadhi) baada ya kukohoa,
• Kuhisi kama kuna kitu kimekwama kooni,
• Kukosa hewa.
1. KWA MTU MZIMA/MTOTO MKUBWA
Mpige kwa kiganja cha mkono mgongoni mara 5. Au simama nyuma yake kisha kunja ngumi na iwe usawa ya chini ya kifua (xiphoid) na mkono mwingine ishikilie ngumi kwa kuvuta kama unakandamiza tumbo (pichani). Pia mtu anaweza kwa kutumia kiti (pichani)
2. KWA MTOTO MCHANGA
Mshike mtoto kama inavyoonesha (pichani). Kisha endelea kumpiga makofi (yasiwe makali sana) mgongoni. Huku ukihakikisha hakosi hewa.
KUMBUKA: Ukiona hali inaendelea au anapata hali ya kukosa hewa; mkimbize hospitali mara moja...
RETWEET.
@jukwaalaafya

Loading suggestions...