Jack upepo
Jack upepo

@kikomasta

12 Tweets 268 reads Feb 26, 2022
CHAZO CHA VITA VINAVYO ENDELEA UKRAINE.(Somewhere in Eastern Europe)
Wengi wanajiuliza why Urusi avamie Ukraine,bila kujiuliza,kuogopa matokeo ya uvamizi kiuchumi.why NATO anajishauri kuingia Ukraine km wanavyo fanya kwny mizozo mingine ya Ulaya.Picha inaanza kaa kwa kutulia =>
Russia ilikuwa ndani ya umoja wa nchi za kisovieti (USSR).Uliokuwa ukijumuisha nchi kama Azebaijan, Armenia, Estonia, Beralus,Ukraine,Latvia,Kazakstan,Tajikistan,Lithuania,Georgia,Moldova,Uzberkistan,sijui kama kuna niliosahau kamaipo ni 1 au 2. ==>
USSR ilikuwa na nguvu kubwa sana Duniani na ulioweza kumzuia Adolf Hitler asiichukue Ulaya mana alishatandika karibu ulaya yote.Baada ya kuvunjika umoja wa nchi za kisoviet(USSR).Ambao kwa kiasi kikubwa ulisababishwa na USA kuhofia nguvu iliyokuwepo kwenye umoja huo.==>
Kama unaijua Cold war utakuwa umepata kitu flani.Russia ilibaki kuwa Russia na nchi nyingine zikabaki zenyewe bila kuwa na umoja wowote.Ingawa umoja ulivunjika lakini % kubwa ya hizi nchi zilikuwa na marais vibaraka wa Russia ama raia bado walikuwa na misimamo ya kirusi.
kitu ambacho kilikuwa ni kutu kwenye chuma cha demokrasia anayosambaza US.Toka hapo pakawa na hofu inawezekana siku moja zile nchi zikajiunga tena na Russia.Au Russia akazichukua kinguvu kurudisha umoja wake ulio vunjika hapo mwanzo.
Hapo likaja wazo la kuzishawishi nchi zilizokuwepo umoja wa USSR wajiunge na umoja wa kujiami wa nchi za ulaya(NATO).Kama utajiunga na NATO jeshi lako litakuwa kubwa na Russia hatoweza kukuchukua kimabavu sababu kuna nchi zitakuwa tayari kuingia vitani kwa ajili yako ukivamiwa.
Hii ilikuwa mbinu ya USA kuhakikisha wanakuwa na ushawishi mkubwa ndani ya Ulaya kumzidi Urusi.Na ku hakikisha Russia haitokuwa na nguvu kama zamani za kumpinga Marekani.Kwenye maamuzi ya kiutawala wa Dunia.Kwakuwa USSR ndio pekee ilikuwa na uwezo wa kumbishia USA
Pamoja na kuvunjika kwa USSR bado Urusi ilikuwa ni nchi pekee inayomiliki mabomu mengi ya nyuklia na masafa marefu zaidi ya USA,Na ya pili kwa uwezo wa Kijeshi baada ya US,Isipokuwa kiuchumi ilikuwa imedondoka vibaya,kuna kipindi ilibidi Marekani aisaidie Urusi kiuchumi.
Kwa kuhofia hali ya Uchumi isije kupelekea Urusi akaanza kuuza Mabomu au teknolojia ya Nyuklia nje ya mipaka.Maisha yaliendelea ingawa mbinu zote za NATO zilijikita zaidi kujikinga na mashambulizi ya Urusi.Kipindi chote hiki Russia ilitazamwa kama Adui anayejipanga taratibu.
Kipindi hich chote Urusi ilichukuliwa kama Mzee mwenye misimamo ya kikoloni iliyopitwa na wakati Mpaka pale Urusi ilipopata huyu mwama Vladmir Putin.Aliye kuwa na dhamila kuleta mabadiliko ya kitechnolojia ya jeshi zima la Urusi kuwa la kisasa na kujikita mahusiano yake na China
Uliozorota kwa muda na kubadili picha nzima ya Urusi kwenye uso wa kimataifa.Kipindi hiki chote Marekani na NATO wanatoa macho kwa Urusi,Wakamsahau China aliyekuwa anakuwa kwa kasi ya ajabu kiuchumi na Kijeshi,mpaka wanastuka China amekuwa hatar zaidi ya Urusi waliyoitolea macho.
Kukua kwa china kulisababisha vipi Kiburi cha Russia kwa NATO na USA.Kwanni kinapelekea ugumu wa NATO na USA kuingilia mzozo wa Ukraine kijeshi muvi itaendelea.Weka like zako na Retweet za kutosha.kwa leo tuishie hapa. #ChafuZamoto #BilaGanzi

Loading suggestions...