HabariTech
HabariTech

@HabariTech

15 Tweets 28 reads Oct 29, 2021
📡METAVERSE (Ulimwengu mpya wa kidijatali)
Metaverse ni muunganiko wa maneno mawili.
Meta – lenye maana ya “Beyond” au “zaidi ya hapo”.
Verse – lenye maana ya “Universe” au “Ulimwengu”.
#HabariTech
📡Metaverse inatambulisha ulimwengu mpya wa kidijitali ambao watu wanaweza kuishi pamoja na unapatikana kupitia internet.
Huu ni uliwengu wa kidijitali ya kwamba haupo katika mazingira ya kweli, upo katika mtandao.
📡Watazamaji wa movie ya “Free Guy” mtaelewa nikisema ni ulimwengu kama ule wa Guy kwenye Free Guy movie.
Au ni sawa na nikisema ulimwengu kama ule wa games za PUBG, CODM au Fortnite kwa gamers. Kwa wengine chukulia twitter kama ndio ulimwengu wenyewe.
📡Sasa metaverse ni ulimwengu ambao unafanana karibu na ukweli kwa kutumia vitu kama Virtual Reality na Augmented Reality.
Ukiacha hii metaverse ya Games za kawaida kuna metaverse ambayo inatumia teknolojia ya Blockchain.
📡Kwenye metaverse hii watu wanaweza kununua mali kama ardhi ya kidijitali na mali nyinginezo kwa kutumia cryptocurrencies.
Umiliki wa mali kidijitali hauishii kwenye ardhi tu. Unaweza miliki hata picha na michoro kwa muundo wa NFT.
📡Muwekezaji mmoja wa Singapore anayejiita “Metakovan” alinunua NFT yenye thamani ya $69 Million kutoka kwa msanii wa Marekani Beeple’s at Chritie’s.
📡Sanaa ya msanii huyu inaitwa “Everydays: The First 5000 Days”. Sanaa hii ni muunganiko wa picha 5000 zilizotengenezwa kwa muda wa siku 5000.
📡Mashabiki wa metaverse wanasema wanaona kwamba hii ndiyo stage inayofata ya ukuaji wa internet. Ni, kweli ndio stage inayofata? Mimi sijui, ila muda utatuambia.
Kwa sasa tunawasiliana kwa kutumia mitandao ya kijamii na jukwaa za meseji kama Twitter na Whatsapp.
📡Wazo la metaverse ni kuleta ulimwengu ambao watu watawasiliana katika mazingira ya multi-dimensional.
📡Fikiria clubhouse, holograms na twitter kuwa kitu kimoja. Namaanisha ulimwengu ambao wewe na mimi tuna avatars zetu zinatembea kwenye uliwmengu wa kidijitali, tunaongea kama kawaida.
📡Yani kama ilivyo Free Guy vile. Utakuwa ni ulimwengu wa aina yake.
Metaverse mpaka sasa inachohitaji ni kuvutia wawekezaji wa kutosha kama kina Mark Zuckerberg.
📡Alafu nikwambie hivi mwezi wa 7 mwaka huu Zuckerberg alisema kwamba ndani ya miaka 5 ijayo facebook itageuka kutoka kuwa mtandao wa kijamii na kuwa metaverse.
Microsoft pia hawajabaki nyuma, wao walisema wanataka kufanya uliwmengu wa kweli na ule kidijitali kuwa kitu kimoja.
📡Unajua kwamba kwenye metaverse wasanii watafanya show zao mtandao wewe utaona kila kitu ukiwa nyumbani?
Hapana, siongelei kuona kama vile show za sasa uanvyoona. Naongelea kuona kwa 3D kwa Virtual Reality. Unajihisi upo kabisa eneo la tukio.
📡Hutaki sasa? Aya sawa kule kwa wahehe huwa wanasema kalaga bao, we twibitaga (we kaa tu hapo sisi tunaenda zetu).
Ni hivi mwezi wa 9 hapo wamiliki wa game ya Fortnite walimlipa Ariana Grande $20 Million ili afanye show ya kidijitali ndani ya game yao. Bado unadhani hii ndoto?
📡Dunia inabadilika hii inakwenda kuwa ya kidijitali kabisa. Ukitaka kuendana nayo anza sasa kujua vitu kama cryptocurrency, NFT, Tokens na Blockchain.
"Muuza madawa huwa hatumii." / "The drug lord never consumes."

Loading suggestions...